Parachichi ni tunda linalopendwa na watu wengi haswa kwa jinsi lilivyo na virutubisho vingi, lakini hata hivyo wataalamu wa afya wameeleza kuwa mbegu iliyo katikati ya parachichi ambayo hutupwa ndio yenye virutubisho maradufu kuliko tunda lenyewe.
Imeelezwa na ‘American Chemical Society’ kuwa ndani ya mbegu hiyo vipo virutubisho ambavyo vinaweza kuwa dawa ya magonjwa ya saratani, magonjwa ya moyo, na kuzuia kukua kwa seli za uvimbe mwilini
Inakadiriwa kuwa duniani kote takriban tani milioni 5 za maparachichi zinazalishwa kila mwaka kiwango ambacho kinaweza kutumika kuleta mapinduzi katika sekta ya afya na dawa kama kutakua na teknolojia nzuri ya kutumia mbegu hizo.
No comments:
Post a Comment