Visiwa vilivyo eneo la Caribbean
vimefanya matayarisho ya mwisho kwa kimbunga Irma, ambacho ni kimbunga chenye
nguvu zaidi kwa mwongo mmoja, huku maafisa wakionya kuwa kimbunga hicho
kinaweza kuwa chenye madhara makubwa.
Kimbunga Irma
cha kiwango cha tano kimepata nguvu ya upepo wa
kasi ya hadi kilomita 295 kwa saa.
Kimbunga hicho kinatarajiwa kupiga visiwa vya Leeward kabla ya
kuelekea huko Puerto Rico, Haiti na Floirda ambapo Watu wameamrishwa kuondoka
kwa lazima eneo la magharibi mwa Florida.
Wageni wametakiwa kuondoka huku wenyeji nao wakitakiwa kunodoka
ifikapo jioni na safari zote za ndege kusitishwa.
Viwanja vya ndege vimefungwa kwenye visiwa kadha, maeneo maarufu
ya kustarehe na mamlaka zimewataka watu kwenda maeneo salama.
Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza hali ya tahadhari huko
Florida, Puerto Rico naa visiwa vya Virgin na kutangaza mikakati ya kukabiliana
na majanga sehemu hizo.
No comments:
Post a Comment