Thursday, September 28, 2017
imeelezwa kuwa mtu anapokubali nguvu ya mungu ingie moyoni mwake anapata nguvu maishani
kauli hiyo imetolewa na mtumishi wa huduma ya ngurumo ya upako mtume rose abel wakati akihubiri katika ibaa ya chuo cha manabii iliyofanyika mchana huu kwenye chuo kikuu cha manabii kisongo arusha.
Tuesday, September 26, 2017
NAIBU WAZIRI WAMBURA AHITIMISHA MASHINDANO YA FLATEI JIMBO CUP MBULU
Halmashauri zote nchini zimetakiwa kutenga maeneo ya michezo wakati wa
kupanga mipango miji kwa matumizi bora ya ardhi katika maeneo yao.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Anastazia Wambura alipokuwa akifunga fainali ya mashindano ya
Jimbo Cup inayodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Mbunge wa
Mbulu Vijijini, Flatei Massay iliyochezwa katika eneo la kata ya Dongobesh
Wilaya ya Mbulu Mkoani wa Manyara.
“Natoa wito kwa Halmashauri zote ikiwemo halmashauri yenu ya wilaya ya
Mbulu wakati wa kupanga matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya mipango miji
mkumbuke kutenga maeneo ya michezo, Baraza la Michezo la Taifa litatoa mafunzo
ya michezo na utaalam” alisema Naibu Waziri Wambura.
Daktari Atoa Uhahidi Mahakamani, Kadai Manji Yupo Hatarini na Anaweza Kufa Muda Wowote
Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Hospitali ya Aga Khan, Mustapha
Bapumia (62) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa anashangaa
mtu mwenye umri mdogo kama Yusuf Manji (41) kuwa na vyuma vinne kwenye
moyo.
Monday, September 25, 2017
Waliomuita Nkosazana Dlamini-Zuma kuwa "mke wa zamani wa Zuma" waomba msamaha
Kituo cha taifa cha habari nchini
Afrika Kusini kimemuomba msamaha mama anayetarajiwa kuwania urais
Nkosazana Dlamini-Zuma, kwa kumuita "mke wa zamani wa Zuma"
Mwanamke aliyetajwa kuwa mwenye uzani mkubwa zaidi duniani amefariki
Mwanamke raia wa Misri ambaye
aliaminiwa kuwa mtu mwenye uzani mkubwa zaidi duniani amefariki kwenye
hospitali moja katika umoja wa falme za kiarabu
Eman Ahmed Abd El Aty alikuwa amepelekwa nchini India kufanyiwa upasuaji wa kupunguza uzito wa mwili.Rais Magufuli Kuongoza Vikao vya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - NEC Kwa Siku Mbili Dar
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Taifa, anatarajia kuongoza
kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kwa siku mbili Jijini Dar es
Salaam, Septemba 30 hadi Oktoba 1, 2017.
Rais Magufuli amemaliza ziara yake ya siku sita katika Mkoa wa Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe
25 Septemba, 2017 amemaliza ziara yake ya siku 6 katika Mkoa wa Arusha.
Waziri wa Afya Aipiga Marufuku Muhimbili kutoa rufaa za nje hata kwa Rais Maguful
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
ametoa agizo kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kuhakikisha haitoi
rufaa ya matibabu nje ya nchi ikiwa wana uwezo wa kutibu maradhi husika
hapa nchini.
NASSARY ADAI ATAJIUUZULU UBUNGE KAMA???????????????
Mbunge
wa Chadema wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari ameweka rehani ubunge
wake baada ya Rais John Magufuli kumpokea aliyekuwa diwani wa chama
hicho aliyejiuzulu akisema ni kwa sababu ya kuunga mkono juhudi za Rais.
Peter Msigwa Kaachiwa kwa Dhamana, Kuripoti kwa RCO Leo
Mbunge
wa Iringa Mjini (Chadema) Msigwa ameachiwa huru jana usiku kwa dhamana
baada ya kukamatwa akiwa kwenye mkutano wa hadhara.
Ndugai: Tundu Lissu ana Bima ya Bunge, Hapaswi Kutibiwa kwa Michango
Spika
wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amefunguka na kudai matibabu ya Mbunge
wa Singida Mashariki Tundu Lissu hayawezi kufanyika kwa kuchangishana
michango kwa kuwa ana bima yake na haki zake ndani ya Bunge.
Utafiti: Yafahamu magonjwa yanayoweza kutibiwa kwa mbegu ya parachichi
Parachichi ni tunda linalopendwa na watu wengi haswa kwa jinsi lilivyo na virutubisho vingi, lakini hata hivyo wataalamu wa afya wameeleza kuwa mbegu iliyo katikati ya parachichi ambayo hutupwa ndio yenye virutubisho maradufu kuliko tunda lenyewe.
Thursday, September 21, 2017
Wednesday, September 20, 2017
Tuesday, September 19, 2017
IBADA YA CHUO KIKUU CHA MANABII.
Watu mbalimbali wamehudhuria ibada ya chuo cha manabii iliyofanyika katika hema la kukutania kisongo Arusha Tanzania, ambapo watu waliohudhuria wamepokea nguvu ya Mungu kutoka kwa watumishi wa Mungu wanaotumika chini ya Nabii mkuu Mh. Dk. GeorDavie.
Pia katika ibada hiyo Gadinali wa kwanza wa huduma ya Ngurumo ya upako Mtume Gaudensia Luila amewakumbusha watu juu ya kuwasilisha michango yao kwa ajili ya kusapoti GeorDavie Tv.
Katika Ibada hiyo chungaji Rispar Asheri amesema ili uweze kupiga hatua katika maeneo mbalimbali ni lazima uwe mnyenyekevu mbele ya Mungu.
NA HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KATIKA IBADA HIYO..
MKURUGENZI MTENDAJI TANECO ALIMWA BARUA YA KUJIELEZA.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani amemtaka Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Dk Tito Mwinuka kuandika barua kujieleza ni kwa nini ameshindwa kuanza ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme cha Kigamboni.
Dk Kalemani ametoa agizo hilo baada ya kutembelea vituo vya kupoozea umeme vya Gongo la Mboto, Kurasini na Kigamboni.
RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI AJALI YA UGANDA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi aliyewahi kuwa Naibu Waziri na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mpwapwa Mkoani Dodoma Bw. Gregory Teu kufuatia vifo vya watu 13 ambao ni ndugu wa familia yake waliopoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea nchini Uganda.
Watu hao wamefariki dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka kwenye sherehe ya harusi kugongana na lori tarehe 17 Septemba, 2017 majira ya saa
Sunday, September 17, 2017
Friday, September 15, 2017
SERIKALI YAUNDA KIKOSI MAALUMU KUDHIBITI MASHAMBILIZI YA RISASI NCHINI.
Wiki moja
baada ya kujeruhiwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu
Lissu Serikali imeunda kikosi kazi kushughulikia uvunjifu wa amani nchini.
Kikosi
hicho kinachoshirikisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama pia kinashughulika
na kukusanya silaha za kivita ambazo zimekuwa zikitumika.
Thursday, September 14, 2017
Wednesday, September 13, 2017
RAIS MAGUFULI AVUNJA MAMLAKA YA UENDELEZAJI WA MJI WA KIGAMBONI (KDA)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amevunja Mamlaka ya uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA) kuanzia leo Septemba 13, 2017.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa amethibitisha hilo na kusema kuwa Rais Magufuli ni msikivu kwani amesikia kilio cha watu wa Kigamboni na
kuamua kuivunja mamlaka hiyo ya Uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA).
kuamua kuivunja mamlaka hiyo ya Uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA).
"Usikivu ni sehemu ya utatuzi hatimaye Rais wa Jamhuli ya Muungano wa
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI GERSON LWENGE
Waziri wa Maji na umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge amesema
Serikali inatekeleza ujenzi wa mradi wa bomba la maji safi kutoka ziwa viktoria
kuelekea katika mji wa Ngudu na vijiji vinavyopitiwa na mradi huo ili kuwapunguzia wananchi adha ya maji
wanayoipata.
Waziri Gerson Lwenge amesema hayo bungeni mjini Dodoma wakati
akijibu swali la Machimba Mashauri Ndaki mbunge wa Maswa Magharibi aliyetaka
kujua
Subscribe to:
Posts (Atom)