Rais
Zuma kwa vipindi mfululizo ameshuhudia maandamano na kura za kutokuwa
na imani zikipigwa kwa lengo la kumtaka ajiuzulu kutokana na tuhuma
mbalimbali za rushwa na upendeleo zinazomkabili.
Kutokana
na kura zilizopigwa jana na bunge la nchi hiyo, jumla ya kura hizo ni
384 huku waliosema hawana imani naye wakiwa 177, wenye imani wakiwa ni
198 na kura zilizoharibika ni 9.
198 na kura zilizoharibika ni 9.
Kwa
mujibu wa matokeo hayo, Wabunge 40 wa chama tawala, ANC wamepiga kura
ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma hivyo kutaka ang’atuke.
Viongozi
mbalimbali wa ANC pamoja na wabunge wengine wa chama hicho, wametaka
wabunge hao (40) wachukuliwe hatua za kinidhamu kwa kile kilichodaiwa
kuwa ni kukisaliti chama.
Muda
mfupi baada ya bunge kutangaza matokeo hayo yaliyokuwa yakisubiriwa kwa
hamu, wafuasi wa Rais Zuma walionekana wakicheza na kuimba kwa furaha
nje ya jengo la bunge wakisherehea ushindi huo.
Aidha,
kwa upande mwingine imeripotiwa kuwa, fedha ya Afrika Kusini (Rand)
imeporomoka kwa zaidi ya asilimia 1 baada ya kutangazwa kuwa Rais Zuma
ameshinda kwenye kura hiyo.
ANC
imempongeza Rais Zuma kufuatia ushindi huo huku kikisema kwamba, mara
zote kimekuwa kikitoa makada wenye kuaminika katika nafasi za serikali.
Rais
Zuma amepigiwa kura ya kutokuwa na imani naye kwa zaidi ya mara 5
ambapo mara zote amefanikiwa kuruka kiunzi na kuendelea kusalia
madarakani.
No comments:
Post a Comment