Tuesday, August 22, 2017

WATU WAALIKWA KUHUDHURIA IBADA YA CHUO CHA MANABII.

Kadinali wa pili wa huduma ya Ngurumo ya Upako mchungaji Elizabeth Humphrey amewaalika watu kuhudhuria ibada ya chuo cha manabii inayofanyika hii leo katika hema la kukutania kisongo Arusha.

Akizungumza na N.Y.U Radio Ofisini kwake Mchungaji Elizabeth Humphrey
amesema kuwa, ni vyema kila mmoja kushiriki ibada hiyo ili kuendelea kujaa neno la Mungu kutoka kwa watumishi wa mungu wanaotumika chini ya nabii mkuu Mh Dk. GeorDavie ambako kila mmoja ataondoka na Baraka ambazo Nabii mkuu amekuwa akiziachilia katika madhabahu.

Huduma ya ngurumo ya upako ibada za katikati ya wiki ni kila siku za Jumanne na Alhamisi ambapo watu kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Arusha hufika katika hema la kukutani kwa ajili ya kupokea uponyaji.

No comments:

Post a Comment