Wednesday, August 16, 2017

SOKO KUU SIDO JIJINI MBEYA LATEKETEA KWA MOTO.



Soko kuu la Jijini Mbeya maarufu kama SIDO limeungua moto usiku wa kuamkia leo .Moto huo ulianza majira ya saa 3 usiku ambapo mali za wafanyabiashara mbalimbali katika soko hilo zimeteketea.

Kwa upande mwingine wananchi wamesikika wakimwaga machozi ya lawama kwa Jeshi la Polisi wakilaumu kutoruhusiwa  kusogea eneo la tukio kuokoa mali zao kwa kuwafyatulia risasi hewani.

Hii ni mara ya tatu sasa ambapo soko hili liliisha ungua mara mbili mfululizo kabla ya  kuungua tena kwa mara nyingine  usiku wa kuamkia leo.
 


No comments:

Post a Comment