Tuesday, August 15, 2017

WATU WOTE WAALIKWA KUHUDHURIA IBADA YA CHUO CHA MANABII.

Kadinali wa pili wa huduma ya Huduma ya Ngurumo ya Upako Mchungaji Elizaberth Humphrey amewaalika watu kutoka sehemu mbalimbali kuhudhuria ibada ya katikati ya wiki inayofanyika hii leo katika hema la kukutania kisongo Arusha.



Akizungumza na N.Y.U Radio ofisini kwake mchungaji Elizaberth Humphreyamesema kuwa katika ibada hiyo watumishi wa mungu hufundisha

neno la mungu kwa kifupi na mara baada ya kufundisha huwafungua watu
kulingana na mahitaji yao.
Pia amesema kuwa ibada za katikati ya wiki ni maono ya Nabii mkuu Mh Dk. GeorDavie ambapo katika ibada hiyo watu hufika katika hema la kukutani
kufundishwa upendo wa Mungu na kutembea katika Nuru ya Kristo.

Huduma ya Ngurumo ya Upako ibada za katikati ya Wiki ni kila siku za Jumanne na Alhamisi ambapo watu kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Arusha hufika katika hema la kukutania kwa ajili ya kupokea uponyaji.

                                                                                                     Habari Na Ngurumo ya Upako.

No comments:

Post a Comment