Raia
wa AfriKa Kusini, Menolaos Tsampos, (61), amefikishwa katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu leo kujibu mashtaka ya kutishia kwa mtandao,
kuishi nchini kwa muda wa miaka minne bila kibali na kutumia paspoti
yenye visa ya kugushi.
Mshtakiwa
huyo ambaye kabla ya kuanza kusomewa mashitaka yake alitishia kuwapiga
waandishi waliokuwa wakimpiga picha kwa kujaribu kurusha mateke na
ngumi.
Amesomewa
mashtaka yake hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha ambapo
amekana mashtaka yote na amerudishwa rumande hadi hapo upande wa
mashtaka utakapothibitisha uhalali wa Visa yake na makazi yake
ya kudumu.
ya kudumu.
Akisoma
hati ya Mashtaka wakili wa serikali, Nassoro Katuga amedai, Juni 22,
mwaka huu ndani ya jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa kwa kutumia mfumo wa
kompyuta, alimuandikia barua pepe Costa Gianna Koulos, yenye maneno ya
vitisho kwa nia ya kumsababishia Koulos hisia za uoga.
Pia
imedaiwa kuwa, Julai 20 Mshtakiwa Tsampos, alimuandikia barua pepe
nyingine Koulos yenye maneno hayo ya vitisho na kumpa masaa 48 kumtaka
wakae na kumaliza tofauti zao kinyume na hapo atamfanyia kitu kibaya. Wakili
Katuga ameendelea kudai kuwa mshtakiwa huyo mwenye pasi ya kusafiria
namba 246184272, raia wa Afrika Kusini, Julai 6, mwaka huu alikamatwa
akiishi nchini bila ya kuwa na kibali maalumu.
Aidha
Agosti 7, mwaka huu katika kituo cha polisi cha Kati, Tsampos, alikutwa
akiwa na pasi ya kusafiria yenye namba M00101612 ikiwa na Visa ya
kughushi.
Mshtakiwa
amekanusha kutenda makosa hayo na amerudishwa rumande baada ya mahakama
kuutaka upande wa utetezi kufanya uchunguzi na kuhakikisha kama kweli
mshtakiwa anaishi mbezi kama ana visa yake. Kesi hiyo imeahirishwa hadi
Agosti 16, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment