Mtu
aliyejitoa mhanga ameua takriban watu 27 kaskazini mashariki mwa Nigeria na
kujeruhi wengine zaidi ya wanane.
Vyombo vya
usalama katika eneo hilo vimesema, watu watatu waliojitoa mhanga akiwemo
mwanamke mmoja, walijilipuwa wenyewe kwenye lango la kuingilia kambi ya
wakimbizi.
Shamabulio hilo lilitokea karibu na mji wa
Maiduguri katika jimbo la Borno, eneo ambalo ni ngome ya kundi lenye itikadi
kali la Boko Haramu.
Karibu watu mia moja hamisini wameuawa katika
mashambulio yanayodaiwa kufanywa na wapiganaji toka kuanza kwa mwezi wa Sita.
Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa Jumatatu
na watafiti wa Kimarekani wanaopinga ugaidi, Boko haramu wamekuwa wakitumia
wanawake na wasichana zaidi kufanya mashambulio kushinda wapiganaji wengine
katika historia.
No comments:
Post a Comment