Tuesday, August 22, 2017

NABII MKUU MH DK. GEORDAVIE ATOA WITO KWA WAKAZI WA KISONGO.

Wito umetolewa kwa wakazi wa kisongo Mkoani Arusha  kujenga hotel  za kisasa sawasawa na neno la kinabii ya kuwa mara baada ya GeorDavie Tv kufanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja wageni kutoka mataifa mbalimbali watakuja kushiriki ibada pamoja na kujifunza mafundisho yanayotolewa  na Nabii mkuu Mh. Dk GeorDavie.

Hayo yamesemwa na Nabii Mkuu Mh Dk. GeorDavie katika kipindi cha kusapoti
magurudumu ya radio ambapo hapo jana ilikuwa ni kusapoti GeorDavie Tv.

Nabii Mkuu Mh Dk. GeorDavie amesema wageni watakaokuja kutoka mataifa mbalimbali watahitaji sehemu nzuri ya kupumzika huku akiongeza kuwa ni vyema wakazi wa kisongo kujenga hotel za kisasa kwa ajili ya wageni hao.

Aidha Nabii Mkuu Mh Dk. GeorDavie  anatarajiwa kuwepo radio siku ya kesho Jumatano kwa ajili ya kusapoti GeorDavie Tv. 

No comments:

Post a Comment