Mbunge
wa jimbo la Kigoma Mjini Mh. Zitto Zuberi Kabwe, amesema pamoja na kuwa
ni mwanasiasa na upinzani na miongoni mwa watu wanaokosoa serikali,
atahakikisha anafanya hivyo pasipo kukamatwa na jeshi la polisi.
Akiwajibu
wananchi kwenye ukurasa wake wa twitter ambao walikuwa wanashangaa kwa
nini yeye hasumbuliwi na polisi licha ya kuongea maneno ya kuikosoa
serikali kama inavyotokea kwa wengine, Zitto Kabwe amesema hataki na
hapendi kufanyiwa hivyo, na atajitahidi kukwepa kitendo hicho.
“Sitaki
na sipendi kukamatwa, itokee kwa kuwa imebidi, lakini kama ipo ndani ya
uwezo wangu kukwepa kukamatwa nitahakikisha sikamatwi”, aliandika Zitto
Kabwe.
Zitto
Kabwe aliendelea kutoa maelezo ya suala hilo akitolea mfano wa viongozi
mbali mbali wa Afrika ambao walikuwa wanaharakati na wanasiasa
waliokuwa wakikososa serikali, lakini hawakuwahi kusumbuliwa kisheria
mpaka ndoto zao zilipotimia.
“Kagame
alikuwa mpiganaji na leo yupo madarakani kwa kuwa hakutaka kukamatwa,
Meles mpiganaji dhidi ya The Derg akiwa na umri mdogo wa miaka 19 mpaka
36 akawa Rais wa Ethiopia 39 hakukamatwa”, aliandika Zitto Kabwe.
Hivi
karibuni mwanasiasa na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu
alikamatwa na polisi kwa kile kilichoelezwa kutoa taarifa za uchochezi.
No comments:
Post a Comment