Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
amemteua Dkt. Hassan Abbas kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari,
Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa
uteuzi wa Dkt. Hassan Abbas umeanza tarehe 09 Agosti, 2017.
Kabla
ya uteuzi huo, Dkt. Hassan Abbas alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari,
Maelezo na aliteuliwa kushika nafasi hiyo na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma
namba 8 ya mwaka 2002.
Dkt.
Hassan Abbas ameteuliwa kushika nafasi hiyo kwa mujibu wa Sheria Mpya
ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016, ambapo nafasi hiyo
imebadilishwa kutoka Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo na kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali
na Mamlaka ya uteuzi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment