Wednesday, August 16, 2017

HATUA ZA KUFUATA ILI KUYAFIKIA MAFANIKIO.



Uvumilivu, hekima na kulishika neno la mungu maishani ni moja ya hatua zitakazomfanya mwanamke kuyafikia malengo aliyojiwekea.

Hayo yamesemwa na wamama wakati wakizungumza katika kipindi cha wamama na majukumu kinachorushwa na N.Y.U Radio kilichokuwa na mada inayosema njia zinazotumika kutimiza malengo.
 

Akichangia mada hiyo kwa upande wake Anna Numi amesema kuwa ili uweze kutimiza malengo uliyopanga ni lazima kumtanguliza Mungu ikiwa ni pamoja na kuhudhuria ibada.

Ameongeza kuwa ili ufikie malengo uliyokusudia ni lazima uchukue hatua pamoja na kuongeza juhudi zitakazokufikisha katika mafanikio.

Kwa upande wake mtumishi Anna Peter Salanje wa huduma ya Ngurumo ya Upako amesema kuwa wamama hawatakiwi kuyakumbuka mambo yaliyopita na badala yake ni vyema kutazama yaliyo mapya ili kuyafikia mafanikio yao.Aidha, Kipindi cha wamama na majukumu hurushwa kila siku ya jumanne kuanzia saa kumi na moja jioni ambapo wamama hujadili mambo mbalimbali yahusuyo familia, kanisa na jamii kwa ujumla.




No comments:

Post a Comment