Naibu
waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Khamis Kigwangala, ameweka wazi sababu ya vijana wengi kufeli
kwenye maisha na kusema kuwa wanapenda kuishi maisha yasiyo na uhalisia.
Kwenye
ukurasa wake wa twitter ambapo alikuwa akijibizana na baadhi ya
watanzania wanaotumia mtandao huo kuhusu tabia ya vijana kutopenda
kujishughulisha na kuchagua kazi, Dkt. Kigwangala amesema vijana wa sasa
hivi wengi wanapenda kuishi maisha ya kwenye mitandao, na kuacha yale
yenye uhalisia na kuweza kujishughulisha kujikwamua kiuchumi, huku
akiweka wazi malipo pekee sio sababu ya vijana wengi kuchagua kazi.
"Siyo
malipo pekee, pia matarjio na matumizi ya vijana, wengi wanataka kuishi
maisha ya 'Instagram' na 'Facebook'...badala ya uhalisia, tamaa ya
maisha mazuri bila kupiga kazi nalo ni tatizo jingine, kubwa tu!", aliandika Dkt. Kigwangala.
Naibu
Waziri Kigwangala aliendelea na mazungumzo hayo na kusema kuwa kwa
jinsi hali ilivyo, kuna haja ya kuweka nguvu yenye ukali ili kuweza
kutatua hali hiyo, na kushawishi vijana wajitambue kuishi maisha yenye
uhalisia.
"Kama
mapambano ni makali zaidi sasa tunapaswa tuandae nguvu na mbinu kali za
kiwango cha ukali uliopo, siyo kukata tamaa, Na huo ndiyo mwanzo wa
tofauti ya waliofanikiwa na wasofanikiwa, kusimama kwenye uhalisia ama
kuleta ubishoo kwenye kazi", aliandika Dkt. Kigwangala.
==>Soma tweet zake hapo chini
No comments:
Post a Comment