Tuesday, August 15, 2017

Rais Kabore na Macron walaani shambulizi la kigaidi jijini Ouagadougou


media 
Hali ilivyokuwa baada ya shambulizi la kigaidi jijini Ouagadougou Reuters
Rais wa Burkina Faso Roch Marc Christian Kabore amelaani shambulizi la kigaidi lilisababisha watu 18 kupoteza maisha jijini Ouagadougou.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron naye pia amelaani mauaji hayo ambayo pia yamesababisha raia mmoja wa Ufaransa kupoteza maisha.
Watu waliokuwa wamejihami kwa silaha walivamia Mkahawa unamilikiwa na raia wa Uturuki na kuanza kuwapiga risasi wateja.
Uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha shambulizi hilo ambalo limezua hali ya wasiwasi jijini Ouagadougou.
Watu walioshuhudia shambulizi hili wamenukuliwa wakisema kwamba watu watatu waliokuwa na bunduki waliwafyatulia risasi wateja waliokuwa nje ya hoteli hiyo.
Kuna wasiwasi kwamba shambulio hilo huenda limetekelezwa na moja ya washirika wa mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda ambao bado wanaendesha shughuli zao katika eneo la Sahel.
Waziri wa mawasiliano wa Burkina Faso Remis Dandjinou amesema haijabainika ni washambuliaji wangapi hasa waliohusika.
CHANZO RFI

No comments:

Post a Comment