Rais
wa China Xijinping amemtaka rais Donald Trump kuchunga mtamshi na
vitendo vinavyozidisha hali ya kuzua wasiwasi ,chombo cha habari cha
kiserikali kimeripoti.
Rais
Trump na Korea Kaskazini wamekuwa wakirushiana cheche za maneno huku
rais huyo wa Marekani akionya kuikabili kivita vikali Korea Kaskazini.
Lakini China ambaye ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini ametaka pande zote mbili kuwa na uvumilivu.
Taarifa ya ikulu ya Whitehouse imesema kuwa Marekani na China zilikubaliana kwamba Korea Kaskazini inatakiwa kusitisha uchokozi
Hofu
kubwa inayoendelea kutanda kuhusu mpango wa kinyuklia wa Korea
Kaskazini ilizidi baada ya taifa hilo kufanyia majaribio makombora yake
ya masafa marefu mnamo mwezi Julai na kisha kutishia kukishambulia
kisiwa kimoja cha Marekani
No comments:
Post a Comment