Zaidi ya watu 500 wametoweka kufuatia maporomoko ya
matope na mafuriko kwa mujibu wa msemaji wa Rais maporomoko hayo
yamesababisha uharibifu mkubwa katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Free
town nchini Sierra Leone.
Siku ya Jumatatu takriban watu 400 wamethibitishwa kufariki baada ya
maporomoko ya matope katika eneo la Regent na mafuriko katika maeneo
mengine mjini Freertown .
Shirika la msalaba mwekundu limeonya kuwa hakuna muda wa kutosha
kuweza kuwaokoa manusura. Mazishi ya pamoja ya waathiriwa yanatarajiwa
kufanyika siku ya Jumatano ili kupunguza idadi ya wafu katika chumba cha
kuhifadhia maiti.
Msemaji wa Rais Abdulai Baraytay aliambia BBC kwamba miili ilikuwa ikitolewa katika matope hayo na vifusi.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa kwamba wafanyakazi wake nchini Sierra
Leone wamekuwa wakisaidia katika juhudi za kuwaokoa manusura.
Chanzo BBC Swahili.
No comments:
Post a Comment