Mtoto
wa miezi sita aliyejeruhiwa na maafisa wa polisi baada ya kutangazwa
kwa matokeo ya uchaguzi yaliozua utata nchini Kenya amefariki, kulingana
na familia yake.
Samantha
Pendo alikuwa mahututi tangu siku ya Ijumaa baada ya kupata majeraha ya
kichwa wakati polisi walipovamia nyumba yao katika mtaa wa mabanda
magharibi mwa mji wa Kisumu.
Babake Joseph Abanja , ameliambia gazeti la Daily Nation: "Nataka haki kwa
mwanangu,hakuwa akiandamana , babake hakuwa akiandamana pia.Mamake hakuwa akiandamana na badala yake walimuua.
mwanangu,hakuwa akiandamana , babake hakuwa akiandamana pia.Mamake hakuwa akiandamana na badala yake walimuua.
''Nilifanya nilivyoambiwa kwenda kupiga kura na kurudi nyumbani'.Walitufuata hapa na kutupiga''.
Takriuban
watu 24 waliuawa katika ghasia ambazo zilizuka baada ya uchaguzi wa
tarehe 8 mwezi Agosti kulingana na shirika moja la haki za kibinaadamu
Kiongozi
wa upinzani Raila Odinga alisema kuwa uchaguzi huo ulifanyiwa
udanganyifu ili kumsaidia rais aliyepo madarakani Uhuru kenyatta
kushinda.
Hatahivyo wachunguzi wa kimataifa wanasema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.
No comments:
Post a Comment