Baadhi
ya madereva wa daladala zinazotumia kituo cha mabasi cha Simu-2000
Mawasiliano kuongezewa ushuru kutoka Sh 500 hadi 1000 wakati wa kutoka
ndiyo sababu mojawapo iliyofanya wagome.
Mbali
na hilo, wamesema ubovu wa barabara hiyo ya Mawasiliano ni sababu
nyingine kwa madai ya kwamba magari yao yanaharibika kila kukicha.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti walisema walianza mchakato huo tangu saa 11
alfajiri na kwamba wataendeleza hatua hiyo hadi mamlaka husika
itakapotoa mwafaka wa sinofahamu.
Mmoja
wa madereva hao Abdulsalum Hamad amesema waliingia katika kituo kama
kawaida lakini wakati wanataka kutoka wakaamriwa kulipa Sh 1000 jambo
ambalo hawakukubaliana nalo.
"Baada
ya kuamua kugoma kutolipa kiasi hiki walitushirikilia kwa nusu saa
ndipo tukachukua uamuzi wa kugoma kabisa na gari itakayoingia hapa kituo
haiwezi kutoka kabisa hadi kieleweke,"amesema Hamad
Kero
nyingi ya muda mrefu waliaamua kuiunganisha katika mgomo huo ni hatua
ya wahusika wa kituo hicho cha kuwatoza faini ga Sh 50000 pindi
wakatapobainika kunawa nyuso wakiwa msalani kwani hawaruhusiwa kufanya
hivyo.
Hamad
aliwataka wahusika wa kituo kuliangalia suala kwa jicho la tatu suala
la tozo ya Sh 1000 kwani huduma zinatolewa na kituo hicho haziendani na
tozo hizo na badala yake waiache ya Sh 500.
No comments:
Post a Comment