Tume huru ya uchaguzi Kenya (IEBC) imemtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne.
Kenyatta amepata kura 8,203,290 na angalau asilimia 25 ya kura katika vituo 35.
Mwenyekiti wa tume hiyo, Wafula Chebukati amekabidhi cheti cha ushindi kwa Kenyatta na mgombea mwenza wake William Ruto.
Akihutubia
jana mara baada yakutangazwa kuwa mshindi, Rais Kenyatta amewashukuru
wananchi kwa kuwa na imani naye na serikali yake.
“Nawaahidi
tutaendelea na kazi tuliyoianza. Nawashukuru sana Kenya. Kadhalika,
naishukuru tume ya uchaguzi kwa kazi nzuri waliyoifanya,” alisema.
“Nawapongeza wote walioshinda, na kwa walioshindwa pia tutaishi kupambana siku nyingine.”
Kwa upinzani alisema: “Sisi
si maadui, ni raia wa nchi moja. Kila shindano, kutakuwa na washindi na
wanaoshindwa, lakini tutasalia kuwa Wakenya. Nawapa moyo wa
ushirikiano, twafaa kuungana pamoja. Wakenya wanataka sisi tufaulu.”
“Sana
kwa Raila Odinga, namuomba yeye, wafuasi wake, wote waliochaguliwa
kupitia upinzani, tutafanya kazi pamoja, tutashirikiana, tutakua pamoja
na kuendeleza nchi pamoja.”
“Kwa
Wakenya wenzangu, uchaguzi huja na kuondoka lakini Kenya itaendelea
kuwepo, tukumbuke daima kwamba sisi ni ndugu na dada. Jirani yako bado
ni jirani yako. Tuendelee kudumisha amani. Hakuna haja ya fujo, sisi
wanasiasa pia huja na kuondoka. Lakini jirani yako atabaki.”
No comments:
Post a Comment