Kiongozi wa Korea Kaskazini
amepokezwa habari kuhusu mpango wa taifa hilo wa kutaka kurusha kombora
hadi katika kisiwa cha eneo la pacific cha Guam kinachomilikiwa na
Marekani kulingana na ripoti za vyombo vya habari.
Lakini ripoti
hiyo imesema kuwa itachunguza vitendo vya Marekani kabla ya kuchukua
hatua ya kurusha kombora hilo katika kisiwa cha Guam.
Wiki
iliopita, Korea Kaskazini ilionya kwamba mikakati inawekwa kushambulia
eneo ambalo ndege za kijeshi za Marekani zimekita kambi.
Kumekuwa na cheche za maneno kati ya Marekani na Korea kaskazini.
Ripoti hiyo ya kitengo cha habari cha KCNA ilisema kuwa Kim Jong
un aliutazama mpango huo kwa muda mrefu na kuujadili na maafisa wakuu
wa
jeshi.
Kamanda wa jeshi la kimkakati la Korea Kaskazini sasa anasubiri agizo baada ya kuandaa shambulio hilo la Guam.
Lakini
ripoti hiyo pia imeongezea kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini
atachunguza mienendo ya Marekani kabla ya kutoa uamuzi wowote, hatua
inayoonekana kupunguza kasi ya cheche za maeneo kati ya mataifa hayo
mawili.
Mwandishi wa BBC Yogita Limaye mjini Seoul anasema kuwa
hatua hiyo itapunguza wasiwasi na kuzuia mgogoro wa kijeshi katika eneo
la Korea.
Mwandishi mwengine ameongeza kuwa baada ya siku kadhaa za vitisho
kutoka Pyongyang ,inaonekana kwamba rais Kim Jong Un sasa anataka
kunyamaza na kutazama hali ,lakini katika taifa lenye siri kubwa kama
Korea Kaskazini huwezi kuwa na hakika.
Wachanganuzi wanasema
inamaanisha kwamba Pyongyang haiko tayari kutekeleza shambulio katika
kisiwa cha Guam, kwa hivyo huenda inachukua muda.
Hatua hiyo
inajiri baada ya waziri wa ulinzi nchini Marekani James Mattis kuonya
kwamba shambulio lolote linaweza kusababisha vita vikali, na iwapo
Pyongyang itarusha kombora kuelekea Guam basi ''itakuwa vita''.
Ameambia
maripota kwamba Jeshi la Marekani litatetea taifa hilo kutoka kwa
shambulio lolote wakati wowote na kutoka kwa taifa lolote.
Pia aliwahakikisha raia wa Guam ,ambapo kuna kambi za kijeshi za
Marekani kwamba takriban watu 160,000 wanalindwa na akasema iwapo
kombora litarushwa ''tutalitibua''.
Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment