Liverpool imekubali kuilipa Arsenal
dau la £40m kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Alex Oxlade
Chamberlain.
Mchezaji huyo mwenye
umri wa miaka 24 ambaye alikataa uhamisho wa Chelsea siku ya Jumanne baada ya
makubaliano kuafikiwa, atajiunga na Liverpool kwa kandarasi ya miaka mitano
ambapo atakuwa akipokea £120,000 kwa wiki.
Oxlade Chamberlain
ambaye yuko mwaka wake wa mwisho wa
kandarasi na Arsenal, alikataa mkataba mpya
ambao angekuwa akilipwa £ 180,000 kwa wiki katika uwanja wa Emirates.
Ameanzishwa mechi
zote nne za Arsenal msimu huu.
Kiungo huyo wa kati
anatarajiwa kufanyiwa ukaguzi wa matibabu kabla ya kuelekea Malta na Uingereza
siku ya Alhamisi kabla ya dirisha la uhamisho kukamilika.
Oxlade Chamberlain
ameichezea klabu hiyo mara 198 tangu ajiunge naye kutoka Southampton mnamo
mwezi Agosti 2011, akifunga mabao 20.
Kitita hicho
kingevunja rekodi ya usajili wa Liverpool, lakini timu hiyo imekubali kumsajili
mchezaji wa RB Leipzig Naby Keita msimu ujao kwa kitita cha £48m.
Kufikia sasa
Liverpool imemsajili winga Mohammed Salah kutoka Roma kwa £34m, beki Andrew
Robertson kutoka Hull kwa £8m na mshambuliaji Dominic Solanke baada ya
kandarasi yake katika klabu ya Chelsea kuisha.
No comments:
Post a Comment