Tuesday, August 1, 2017

HAPPY ALLAN:KUTII NA KUNYENYEKEA NI NJIA BORA YA KUPATA BARAKA KWA MUNGU.

Kuwa mtii na kukubali kunyenyekea ni mojawapo ya njia ya kuweza kupata baraka kwa mungu kupitia watumishi wake .
Hayo yamesemwa na watumishi wa mungu mchungaji  mwanafunzi wa watoto  happy allan pamoja na  mwinjilisti uwela mpinga wakati wakihubiri katika ibada ya chuo cha manabii iliyofanyika hii leo ndani ya chuo kikuu cha manabii.

Mchungaji wa watoto happy allan amesema kuwa kujipa moyo na kuwa mnyenyekevu kwa Mungu inasaidia  kufanikiwa katika mambo mbalimbali
katika maisha.

Kwa upande wake mwinjilisti uwela mpinga  amesema kuwa bwana anawawazia watu wote  yaliyo mema ndio maana watu huuona upendo wa mungu katika maisha yao.

Watu waliohudhudhuria ibada ya leo wamefurahishwa kwa kuuona uwepo wa mungu huku wakiwashauri watu wengine kuhudhuria ibada za katikati ya wiki.



No comments:

Post a Comment