Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea
kuwaonya Watanzania wenye tabia ya uvivu na kupenda kubweteka bila
kujituma, huku akisema wakati wa utawala wake hakutakuwa na vitu vya
bure.
Rais
Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akihutubia wananchi wa wilaya ya
Korogwe mkoani Tanga waliohudhuria uzinduzi wa kituo cha mabasi (Stand)
wilayani humo, na kusema kuwa watu wanaopenda kukaa vijiweni bila
kujishugulisha huku wakilalamika njaa na hakuna pesa, ni bora wafe na
njaa.
"
Wakati wa kukaa kwenye magenge na kupiga maneno umepitwa na wakati,
mnakaa kwenye pool unasubiri vitakuja hakuna, vya namna hiyo nataka
kuwaeleza havitakuja kwenye utawala wangu, mnakaa mnasubiri tuna njaa
tunataka mtuletee, mimi njaa nafuu ikuue kuliko nikuletee chakula, kwa
sababu kama mwenzako ana chakula wewe una njaa, hatuwezi tukavumilia
vitu vya namna hiyo", alisema Rais Magufuli.
vitu vya namna hiyo", alisema Rais Magufuli.
Rais
Magufuli aliendelea kusema ni lazima awaeleze Watanzania ukweli kuhusu
hilo, bila kujali kuchukiwa kwani atasimamia haki huu akiwa na dhamira
ya kwenda mbele.
"Ni
lazima niwaeleze ukweli, nafuu mnichukie lakini niwaeleze ukweli,
lakini hata mkinichukia hata sura yangu wala haipendezi, lakini mimi
nitasimamia haki ya kuwaeleza ukweli, tunataka twende mbele, tunataka
tubadilishe nchi, serikali itafanya juhudi zake zote kuwasaidia
Watanzania", alisema Rais Magufuli
No comments:
Post a Comment