Tume ya Uchaguzi nchini Rwanda inasema kuwa Paul Kagame ameshinda uchaguzi wa uraisi uliyofanyika jana nchini humo.
Tume
hiyo imesema matokeo ya awali yameonyesha kuwa Rais Kagame alishinda
kwa asilimia 98 ya kura zilizohesabiwa. Rais Kagame ambaye amekuwa
madarakani kwa miaka kumi na saba sasa atahudumu muhula wa tatu wa miaka
saba.
Wafuasi
wake wanamsifu Kagame kwa kuleta utulivu na maendeleo ya kiuchumi
nchini humo baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo maelfu ya
watu waliuaawa.
Wapinzani wa bwana Kagame walikuwa ni Frank Habineza na Philippe Mpayimana
Rais
Kagame aliingia madarakani mwaka 1994 wakati kundi lake la waasi
lilichukua udhibiti wa mji mkuu Kigali na kukomesha mauaji ya kimbari
ambapo watu 800,000 watusi na wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa.
Katiba ya Rwanda ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2015 na kumpa Kagame fursa ya kusalia madarakani hadi mwaka 2034.
Wapinzani
wa Kagame wamelalamika kuwa wafuasi wao wanahangaishwa, wakisema kuwa
ndiyo imesababisha kuwepo watu wachache katika mikutano yao ya kabla ya
kura. Hata hivyo chama tawala kimekana madai hayo.
No comments:
Post a Comment