Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametembelea na kujionea mtambo wa kisasa wa
kusafisha dhahabu kwa asilimia 99 unaomilikiwa na kampuni ya Sunshine
Group uliopo katika kata ya Matundasi wilayani Chunya mkoani Mbeya.
Ametembelea
mtambo huo jana (Jumanne, Agosti 1, 2017) wakati akiwa katika ziara
yake ya kikazi mkoani Mbeya na kusema kuwa mtambo huo ni wa kwanza
kuweza kusafisha dhahabu kwa kiwango hicho hapa nchini.
Alisema
kwa Tanzania kampuni ya Sunshine Group ndiyo yenye mtambo wa kuweza
kusafisha dhahabu na kufikia asilimia 99 ukilinganisha na makampuni
mengine yanayomiliki migodi.
Pia Waziri Mkuu alisema Serikali inaendelea kufanya mazungumzo na makampuni mbalimbali kwa ajili ya kuwekeza katika mradi wa ujenzi wa mtambo wa kuchenjulia makinikia ili kuweza kusafirisha dhahabu halisi.
Naye
Ofisa Madini Mkoa wa Mbeya, Mhadisi Said Makwama alisema dhahabu
inayosafishwa katika mtambo huo ikipelekwa nje ya nchi inaingizwa sokoni
moja kwa moja tofauti na migodi mingine.mengine yanayomiliki migodi.
Pia Waziri Mkuu alisema Serikali inaendelea kufanya mazungumzo na makampuni mbalimbali kwa ajili ya kuwekeza katika mradi wa ujenzi wa mtambo wa kuchenjulia makinikia ili kuweza kusafirisha dhahabu halisi.
Mhandisi huyo alisema Sheria mpya ya Madini imesaidia Serikali kupata kodi ya juu itokanayo na Mrabaha wa asilimia 6 na ‘clearance and inspection fee’ ya asilimia moja ya thamani ya madini yanayosafirishwa ukilinganisha na mrabaha wa awali wa asilimia nne.
“Uzalishaji
uliofanyika kwa mwezi Julai tu Serikali imepata mrabaha wa sh. milioni
333 ukilinganisha na sheria ya zamani Serikali ingepata shilingi milioni
191. Sheria mpya imewezesha Serikali kupata mapato zaidi ya sh. milioni
142. Awali ilikuwa inapata sh. milioni 191 kwa gramu 52. 518 kwa mgodi
mmoja wa Sunshine.”
Kwa
upande wake mbunge wa Chunya, Mheshimiwa Victor Mwambalaswa ameiomba
Serikali kukubali maombi ya Kampuni ya Sunshine ya kujenga mtambo wa
kuchenjulia mabaki ya mchanga wa dhahabu wilayani Chunya ili kuweza
kuongeza fursa za ajira, ambapo Waziri Mkuu amesema suala hilo
linashughulikiwa.
Awali
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Sunshine Group Bw Leo Le alisema kampuni
ya Sunshine Group ni ni miongoni mwa makampuni makubwa kutoka nchini
China yaliyowekeza Tanzania, ambapo thamani ya uwekezaji wao ni zaidi ya
Dola za Marekani milioni 100.
No comments:
Post a Comment