Kwa
mujibu wa vyombo vya usalama nchini humo, Musando alifanya mawasiliano
ya mwisho Jumamosi majira ya saa tisa alfajiri ambapo alituma ujumbe
mfupi kwa mmoja kati ya wafanyakazi wake.
Jeshi
la polisi nchini humo limesema kuwa mwili wa Musando ulipatikana pamoja
na mwili wa mwanamke mwingine ambaye hakutambulika mapema na kisha
kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti jijini humo.
Marehemu
alikuwa na jukumu la kusambaza vifaa vya kielektroniki ambavyo
vitatumika kuwatambua wapiga kura na kusambaza matokeo ya uchaguzi mkuu
kutoka katika vituo vya kupigia kura.
Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi kutoka kwa vyombo vya usalama kuhusu upelelezi wa tukio hilo na yaliyomkuta Musando.
Kenya
inatarajia kufanya uchaguzi mkuu Agosti 8 mwaka huu, uchaguzi unaotajwa
kuwa wa ushindani zaidi katika historia ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment