Utawala wa rais Donald Trump
umechagua makampuni manne kwa kazi ya kujenga sampuli ya ukuta ambao
rais Trump ulitangaza sana juu ya mpaka wa Mexico na nchi yake.
Thursday, August 31, 2017
Harbinder Sethi wa Escrow kawekewa Maputo tumboni
Wakili
wa mshtakiwa Harbinder Sethi, Joseph Makandege ameulalamikia upande wa
Jamhuri kwa kushindwa kumpeleka mteja wake Hospitali ya Taifa Muhimbili
kama Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilivyoamuru.
Rugemalira wa Escrow agonga mwamba Mahakama ya Mafisadi
Mshtakiwa
wa kesi ya uchotaji fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow, James
Rugemalira amegonga ukuta katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya
Rushwa na Uhujumu Uchumi (Mahakama ya Mafisadi) baada ya kunyimwa
dhamana.
Rugemalira
ambaye anakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,
yenye mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana, alikimbilia
mahakamani hapo kuomba afutiwe mashtaka ya utakatishaji fedha kisha
aachiwe huru kwa dhamana kwa madai hati ya mashtaka yanayowakabili ina
kasoro za kisheria.
Jana,
Jaji Mfawidhi Firmin Matogolo alitupilia mbali maombi hayo akisema
Mahakama hiyo haina mamlaka ya kumpa nafuu alizokuwa akiziomba.
Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Makongoro Mahanga Akamatwa kwa Amri ya Mahakama Kuu
Mbunge
wa zamani wa Ukonga na Segerea, Dk Makongoro Mahanga amekamatwa na
Polisi Mkoa wa Ilala kwa amri ya Mahakama Kuu na amefikishwa mahakamani.
KUWENI NA IMANI KWA MUNGU.
BALOZI WA NABII MKUU TANZANIA MTUME SEKELA N'TONDOLO
watu wametakiwa kuwa na imani kwa mungu kupitia
watumishi wake anaowatumia kwani itawasaidia kufanikiwa katika mambo mbalimbali maishani .
Wednesday, August 30, 2017
WATU WAKUMBUSHWA KUFIKA HEMAINI MWA BWANA.
Kadinali wa pili wa huduma ya
ngurumo ya upako mchungaji Elizabeth Hamphrey amewakumbusha watu wote
kuhudhuria ibada ya Baraka ya chuo cha manabii itakayofanyika siku ya kesho
katika hema la kukutania kuanzia saa sita kamili mchana.
Akizungumza na N.Y.U Radio Mchungaji Elizabeth Humphrey amesema kuwa ni
vyema kila mmoja kufika mbele za bwana ili kufundiswa neno la Mungu ikiwa ni
LIVERPOOL KUMSAJILI OXLADE CHAMBERLAIN.
Liverpool imekubali kuilipa Arsenal
dau la £40m kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal na Uingereza Alex Oxlade
Chamberlain.
Mchezaji huyo mwenye
umri wa miaka 24 ambaye alikataa uhamisho wa Chelsea siku ya Jumanne baada ya
makubaliano kuafikiwa, atajiunga na Liverpool kwa kandarasi ya miaka mitano
ambapo atakuwa akipokea £120,000 kwa wiki.
Oxlade Chamberlain
ambaye yuko mwaka wake wa mwisho wa
Tuesday, August 29, 2017
BUNGE LA CHINA LAUWEKEA SHERIA WIMBO WA TAIFA.
Bunge la China linatafakari juu ya
rasimu ya sheria ambayo itarasimisha kuwa ni kosa la jinai linalostahili hukumu
ama kifungo juu ya tabia ya kudharau wimbo wa kitaifa wa nchi hiyo.
Kosa kubwa zaidi
litakalochukuliwa kama uhalifu mkubwa ni kwa wale,
WAFUNGWA KUPATIWA KAZI MAGEREZA KWA MIKATABA MAALUMU
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameliagiza jeshi la Magereza na idara zingine zenye mashirika ya uzalishaji ambazo zipo chini ya wizara yake zifanye uzalishaji mali pamoja na kuwatumia wafungwa katika kufanya kazi ndani ya jeshi.
Waziri Nchemba ameongea hayo akiwa katika ufunguzi wa nyumba tano za
Monday, August 28, 2017
BODABODA WASIOVAA KOFIA NGUMU KUKAMATWA.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuwakamata wamiliki wapikipiki ambao watashindwa kuwa na kofia ngumu za pikipiki maarufu kama bodaboda.
Waziri Mwigulu ameyaongea hayo akiongea na madareva wa pikipiki wa wilaya ya shinyanga ambao wanapatiwa mafunzo ya usalama barabarani mkoani
POLISI, JAJI MKUU WATOA ONYO KUHUSU MGOMO WA MAWAIKILI NCHINI
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na Jeshi la Polisi nchini, wamelionya Baraza la Uongozi la Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), kutoingilia vyombo vya uchunguzi na upelelezi, vinavyochunguza tukio la mlipuko, uliotokea kwenye ofisi za Kampuni ya Mawakili ya IMMMA usiku wa kuamkia juzi jijini Dar es Salaam.
Profesa Juma jana alisema TLS hawana haki ya kutoa agizo kwa mawakili, kutohudhuria mahakamani na kwenye mabaraza mengine, kwa kuwa kila wakili ana mkataba binafsi na mteja wake.
POLISI SINGIDA WAUA MTU MMOJA AKIDAIWA KUWA JAMBAZI.
Mkazi wa kijiji cha Shiponga, Hanang Mkoani Manyara anayedaiwa kuwa jambazi, Hamisi Athumani (32), amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kiunoni na askari polisi wakati akiwa katika harakati ya kutoroka.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa, ACP Debora Magiligimba, amesema tukio hilo limetokea Agosti 25 mwaka huu saa nane mchana, huko katika kijiji cha Mgori tarafa ya Ngimu wilaya ya Singida.
Sunday, August 27, 2017
Saturday, August 26, 2017
Zitto Kabwe Aeleza Kwa Nini Yeye Hakamatwi na Polisi Licha ya Kuikosoa Serikali
Mbunge
wa jimbo la Kigoma Mjini Mh. Zitto Zuberi Kabwe, amesema pamoja na kuwa
ni mwanasiasa na upinzani na miongoni mwa watu wanaokosoa serikali,
atahakikisha anafanya hivyo pasipo kukamatwa na jeshi la polisi.
Akiwajibu
wananchi kwenye ukurasa wake wa twitter ambao walikuwa wanashangaa kwa
nini yeye hasumbuliwi na polisi licha ya kuongea maneno ya kuikosoa
serikali kama inavyotokea kwa wengine, Zitto Kabwe amesema hataki na
hapendi kufanyiwa hivyo, na atajitahidi kukwepa kitendo hicho.
“Sitaki
na sipendi kukamatwa, itokee kwa kuwa imebidi, lakini kama ipo ndani ya
uwezo wangu kukwepa kukamatwa nitahakikisha sikamatwi”, aliandika Zitto
Kabwe.
Zitto
Kabwe aliendelea kutoa maelezo ya suala hilo akitolea mfano wa viongozi
mbali mbali wa Afrika ambao walikuwa wanaharakati na wanasiasa
waliokuwa wakikososa serikali, lakini hawakuwahi kusumbuliwa kisheria
mpaka ndoto zao zilipotimia.
“Kagame
alikuwa mpiganaji na leo yupo madarakani kwa kuwa hakutaka kukamatwa,
Meles mpiganaji dhidi ya The Derg akiwa na umri mdogo wa miaka 19 mpaka
36 akawa Rais wa Ethiopia 39 hakukamatwa”, aliandika Zitto Kabwe.
Hivi
karibuni mwanasiasa na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu
alikamatwa na polisi kwa kile kilichoelezwa kutoa taarifa za uchochezi.
Tembo Avamia Kijiji......Aua Mtu Mmoja Kwa Kumkanyaga na Kujeruhi Mwingine
Kijana
Emmanuel Ernest wa kitongoji cha Ilolo, Mvumi Misheni wilaya ya
Chamwino Mkoani Dodoma, amefariki dunia baada ya kukanyagwa na tembo
huku mwingine akijeruhiwa vibaya baada ya tembo huyo kuvamia mashamba ya
zabibu.
Rais Magufuli afanya ziara ya kushtukiza Feri Dar na kutoa maagizo kwa RC Makonda
Polisi Yaanza Kuchunguza Mlipuko Ulioteketeza Ofisi za Mawakili Fatma Karume na Lawrence Marsha
Kaimu
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya
amethibitisha kushambuliwa ofisi za wanasheria za IMMMA saa 8 usiku wa
kuamkia leo Jumamosi, Agosti 26.
Friday, August 25, 2017
NDUGAI ATOA ONYO KWA WABUNGE WATAKAOFANYA VURUGU BUNGENI.
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema wabunge watakaofanya vitendo vya utovu wa nidhamu bungeni hawatavumiliwa na huenda adhabu ikaongezeka maradufu kwa wasiozingatia kanuni.
Ndugai aliyekuwa nje ya nchi kwa mwezi mmoja akitembelea Nigeria, Dubai na
RAIS MAGUFULI ATAKA WALA RUSHWA WAFUNGWE.
Rais Magufuli, amesema anataka walarushwa wengi wafungwe licha ya kuwa kuna baadhi ya watu hawataki kusikia kauli hiyo.
Hayo aliyasema jana Ikulu Dar es Salaam baada ya kumwapisha Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Brigedia Jenerali John Mbungo.
Alisema wakifungwa walarushwa nchi haitakuwa na rushwa kwani ndio
Thursday, August 24, 2017
WATU WAALIKWA KATIKA IBADA YA CHUO CHA MANABII NGURUMO YA UPAKO
Kadinali wa pili wa huduma ya
ngurumo ya upako Mchungaji Elizabeth Humphrey amewaalika watu wote kuhudhuria
ibada ya chu cha manabii inayofanyika hii leo katika hema la kukutania ngurumo
ya upako kisongo Arusha.
Akizungumza na N.Y.U Radio ofisini
kwake Mchungaji Elizabeth Humphrey amesema kuwa ni vyema kila mmoja kushiriki
ibada ili kuendelea kujaa neno la mungu kutoka kwa watumishi wa mungu
wanaotumika chini ya nabii mkuu Mh
Tuesday, August 22, 2017
WATU WAALIKWA KUHUDHURIA IBADA YA CHUO CHA MANABII.
Kadinali wa pili wa huduma ya Ngurumo ya Upako mchungaji
Elizabeth Humphrey amewaalika watu kuhudhuria ibada ya chuo cha manabii inayofanyika
hii leo katika hema la kukutania kisongo Arusha.
Akizungumza na N.Y.U Radio Ofisini kwake Mchungaji Elizabeth
Humphrey
NABII MKUU MH DK. GEORDAVIE ATOA WITO KWA WAKAZI WA KISONGO.
Wito umetolewa kwa wakazi wa kisongo Mkoani Arusha kujenga hotel
za kisasa sawasawa na neno la kinabii ya kuwa mara baada ya GeorDavie Tv
kufanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja wageni kutoka mataifa mbalimbali watakuja
kushiriki ibada pamoja na kujifunza mafundisho yanayotolewa na Nabii mkuu Mh. Dk GeorDavie.
Hayo yamesemwa na Nabii Mkuu Mh Dk. GeorDavie katika kipindi
cha kusapoti
SERIKALI KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI KUDHIBITI AJALI BARABARANI.
Serikali
imetoa mwezi mmoja kwa Mamlaka zinazohusika na masuala ya usalama
barabarani kuhakikisha zinakamilisha uboreshaji wa mfumo wa
kielektroniki wa uwekaji wa vifaa vya kufuatilia udhibiti mwendo
barabarani ikiwa lengo ni kushughulikia matatizo ya kiusalama barabarani
kupitia vyombo vya usafiri.
Akizungumza
hayo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
MWALIMU WA SHULE YA MSINGI AMBAKA MWANAFUNZI NA KUMSABABSHIA UJAUZITO.
Mwalimu
wa shule ya msingi katika kata ya Ligunga tarafa ya Matemanga wilaya
Tunduru mkoani Ruvuma Rajabu Morisi amefikishwa katika Mahakama ya
wilaya hiyo kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake na kumsababishia
ujauzito.
IGP SIRRO AZUNGUMZIA SAKATA LA MIILI YA WATU KUKUTWA KWENYE VIROBA KATIKA FUKWE ZA BAHARI YA HINDI.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amezungumzia suala la
kuokotwa miili ya watu kwenye viroba katika fukwe za bahari ya Hindi, na
kusema suala hilo tayari lipo mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa
uchunguzi zaidi.
Sirro
amesema kweli taarifa hizo zimelifikia Jeshi la Polisi, na kwamba
tayari miili ipo
IBADA LIVE YA CHUO CHA MANABII.
Sikiliza ibada ya chuo cha manabii moja kwa moja kupitia N.Y.U RADIO 99.3 na kupiti www.nyufmradio.radio12345.com
MAJENGO 22 YA ZAHANATI YAKOSA WATUMISHI NA VIFAA TIBA MBEYA.
Majengo 22 yaliyojengwa na wananchi kwa
makusudi ya kutumika kama zahanati katika halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa
miaka minne sasa, hayatumika kwa kukosa watumishi na vifaa tiba.
Monday, August 21, 2017
Rais Buhari asisitiza umoja hotuba ya kwanza baada ya kurejea Nigeria
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameihutubia taifa baada ya kuwa Uingereza kwa miezi mitatu akipata matibabu.
Jenerali wa Jeshi Ateuliwa na Rais Magufuli Kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU
Raisi
John Magufuli leo August 21, 2017 amemteua Brigedia Jenerali John
Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Madereva Daladala Kituo cha Simu 2000 Wagoma
Baadhi
ya madereva wa daladala zinazotumia kituo cha mabasi cha Simu-2000
Mawasiliano kuongezewa ushuru kutoka Sh 500 hadi 1000 wakati wa kutoka
ndiyo sababu mojawapo iliyofanya wagome.
Sunday, August 20, 2017
Friday, August 18, 2017
MAKAMU WA RAIS AWASILI NCHINI AFRIKA KUSINI KUMUWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KATIKA MKUTANO WA 37 WA SADC.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili
nchini Afrika ya Kusini tayari kwa kuhudhuria Mkutano wa 37 wa Wakuu wa
Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC
unaoaanza tarehe 19 na 20 ambapo kesho tarehe 18 atahudhuria Mkutano wa
Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC
Double Troika Summit).
POLISI WATIBUA JARIBIO LA PILI LA SHAMBULIZI UHISPANIA.
Maafisa wa polisi wa
Uhispania wanasema kuwa wamewaua watu watano katika mji wa Cambrils ili kuzuia
jaribio la pili la shambulio baada ya shambulio la hapo awali kufanyika mjini
Barcelona.
Washambuliaji
walikuwa wamevalia vilipuzi , polisi wamesema.
Watu 13 walifariki
huku makumi wakijeruhiwa baada ya gari dogo kuingia katika eneo la watu mjini
Barcelona eneo la Las Ramblas siku ya alhamisi mchana
Thursday, August 17, 2017
AKAMATWA NA POLISI KWA KUMPAKA MWANAE KINYESI.
Mtu
mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kumfanyia ukatili
mtoto wake wa kumpaka mavi ya mbuzi kwenye majeraha aliyoungua na moto
wilayani Nyamagana.
Kwamba
tarehe 15.08.2017 majira ya saa 16:30hrs jioni katika Mtaa wa
Chakechake – Mkuyuni Wilaya ya Nyamagana Jiji na Mkoa wa Mwanza,
Sospeter Rajabu miaka 42, mvuvi na mkazi wa mtaa wa Chakechake –
Mkuyuni, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumfanyia ukatili
mtoto wake aitwaye Neema Sospeter miaka 10, mwanafunzi wa darasa la
kwanza, kwa kumpaka mavi ya mbuzi kwenye majeraha ya moto aliyoungua
maeneo ya mapaja ya miguu yote miwili kwa muda wa wiki mbili na
kupelekea majeruhi kuwa na hali mbaya kiafya, kitendo ambacho ni kinyume
na sheria.
MAPOROMOKO YASITISHA MAISHA YA WENGI NCHINI SIERRA LEONE.
Zaidi ya watu 500 wametoweka kufuatia maporomoko ya
matope na mafuriko kwa mujibu wa msemaji wa Rais maporomoko hayo
yamesababisha uharibifu mkubwa katika maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Free
town nchini Sierra Leone.
Wednesday, August 16, 2017
MTOTO MCHANGA WA MIEZI 6 ALIYEJERUHIWA NA POLISI AFARIKI DUNIA.
Mtoto
wa miezi sita aliyejeruhiwa na maafisa wa polisi baada ya kutangazwa
kwa matokeo ya uchaguzi yaliozua utata nchini Kenya amefariki, kulingana
na familia yake.
Samantha
Pendo alikuwa mahututi tangu siku ya Ijumaa baada ya kupata majeraha ya
kichwa wakati polisi walipovamia nyumba yao katika mtaa wa mabanda
magharibi mwa mji wa Kisumu.
Babake Joseph Abanja , ameliambia gazeti la Daily Nation: "Nataka haki kwa
MARUFUKU BODABODA KUBEBA WANAFUNZI NA WATOTO CHINI YA MIAKA 10 .
Jeshi
la Polisi August 15, 2017 limetoa tamko la kupiga marufuku Waendesha
Bodaboda kubeba watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 na kwamba
atakayekiuka agizo hilo pamoja na mzazi aliyeruhusu mwanawe kubebwa
watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na faini, kifungo au
vyote viwili.
Subscribe to:
Posts (Atom)