Kampuni
ya Barrick Gold ya nchini Canada, imesema wiki ijayo timu ya wataalamu
wake watakuja nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzao na Serikali kuhusu
uendeshaji wa migodi yake.
Tamko
hilo limekuja siku chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kutangaza
kuwa iwapo Barrick inayoimiliki Kampuni ya Acacia itachelewa kuja
kufanya mazungumzo ataifunga migodi yao.
Wakati
kampuni hiyo ikijiandaa kuja nchini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
tayari imepeleka madaia ya Dola za Marekani bilioni 190 ambazo ni sawa
na Sh trilioni 424), kwa Kampuni ya Acacia, ikiwa ni malimbikizo ya kodi
kutoka mwaka 2000.
Taarifa
iliyochapishwa kwenye mtandao wa Financial Post juzi ilisema. “Kampuni
ya Barrick Gold kupitia ripoti yake ya robo mwaka imesema itaanza
majadiliano na Serikali ya Tanzania wiki ijayo kuhusu marufuku ya
kusafirisha nje madini na
masuala mengine yaliyoikumba kampuni inayoimiliki ya Acacia.
masuala mengine yaliyoikumba kampuni inayoimiliki ya Acacia.
“Taarifa
hiyo ya mazungumzo inakuja baada ya Jumatatu wiki hii Tanzania
kuwasilisha bili ya dola bilioni 190 kwa Accacia yenye makao makuu
Uingereza.
“Serikali
ya Tanzania inaituhumu Acacia, ambayo inamilikiwa na Barrick kwa
asilimia 63.9 kudanganya mapato yake ili kukwepa kodi na hivyo kuitaka
ilipe malimbikizo pamoja na faini. Acacia imekana tuhuma hizo.
“Tanzania
pia iliweka marufuku ya kusafirisha mchanga wa dhahabu (makinikia) na
fedha Machi mwaka huu, hatua ambayo inaweza kuathiri asilimia sita ya
uzalishaji wa wakia milioni 5.3 hadi milioni 5.6 ya dhahabu kwa mwaka
katika migodi ya Acacia.
“Barrick
ilisema inasubiri hadi Acacia itakaporekebisha mwongozo wake wa
uzalishaji kabla ya kubadili mwelekeo mzima wa uzalishaji wake kwa
mwaka,” ilisema taarifa hiyo.
Taarifa
hiyo ilisema, Barrick yenye makao yake makuu Toronto, Canada iliripoti
kuongezeka kwa mapato kufikia Dola bilioni 1.08 robo iliyoishia Juni 30,
kutoka dola milioni 138 kwa mwaka mwaka jana.
“Hilo
lilichochewa na mafanikio makubwa ya mauzo ya hisa katika mgodi wa
Veladero na mradi wa Cerro Casale. Mtiririko wa fedha kwa kipindi hicho
ulikuwa dola milioni 43 ukiwa umeshuka kutoka dola milioni 274 kwa
kipindi kama hicho mwaka jana kutokana na kiwango cha juu cha kodi,
ongezeko la mtaji na ongezeko lililopangwa kwa ajili ya matumizi ya
ukuaji wa badaye,” ilisema.
Juni
14 mwaka huu, Rais Magufuli alikutana na kufanya mazungumzo na
Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation Profesa John Thornton
na Ikulu ikatoa taarifa kwa umma kwamba, katika mazungumzo hayo, kampuni
hiyo imesema ipo tayari kufanya mazungumzo na Serikali ya Tanzania ili
kulipa fedha ambazo Tanzania imezipoteza kutokana na kampuni hiyo
kuendesha shughuli zake hapa nchini.
Julai 21, 2017 akizungumza kwenye mkutano wa hadhara mkoani Kigoma, Rais Magufuli alisema.
“Nitasimamia haki siku zote katika maisha yangu, na niliwaambia
nimeanzisha vita hii ya kiuchumi, vita ya kiuchumi ni mbaya sana,
wakubwa wale huwa hawafurahi, kuna viongozi wengi tu mliona yaliyowapata
ni kwasababu nchi zao zilikuwa na mali.
“Lakini
wale wakubwa wakataka kuchezea hizo mali, kwa manufaa yao na siyo kwa
manufaa ya wananchi wa pale, walitumia mbinu nyingi za kila aina, lakini
Mungu wangu ni mwema na Watanzania ni wema watasimama kwa ajili ya
taifa hili.
“Ninayoongea
nayajua ni matrilioni ya fedha ambayo yameibiwa, na kwasasa hivi
tumewaita waje wafanye mazungumzo, wamekubali lakini wakichelewachelewa
nitafunga migodi yote.
“Ni
mara 10 migodi hii tukaigawana Watanzania wachimbe wawe wanauza tuwe
tunapata kodi, kuliko kuchimbwa na watu wanaojiita wawekezaji halafu
hawalipo kodi.
“Walikuwa wanazungumza mle wanachimba dhahabu, madini machache tu, matatu. tumegundua mle kuna madini mengi.
“Tanzania
hii ni nchi tajiri, lakini imekuwa ikiibiwa mno, tumechezewa sana, mimi
nipo serikalini na mimi ndiye najua siri za serikali, tumechezewa sana
kwa kuibiwa sana mali zetu, kwenye dhahabu huku tumeibiwa mno, ukiyajua
yale yaliyokuwa yanafanyike mle unaweza ukalia.
“Unaweza
ukatamani usiishi, mtu anachimba anapokea anapeleka na anashirikiana na
baadhi ya watu tuliowaamini kwenda kulisimamia hili.
“Anasema
hapa tunasafirisha mchanga na Watanzania wote tunaamini tunasafirisha
mchanga, mbona hawajaja Kibondo kuchukua mchanga wa hapa mbona na
penyewe tunao?
“Lakini
tunaamini, wanaupeleka kwenye makontena wanapeleka Ulaya na wakisha
enda kuusafisha kule ule mchanga unaobaki wala hawaurudishi, ulikuwa ni
utapeli wa ajabu, na ni aibu kubwa kuona utapeli huu unafanywa na watu
ambao ni wakubwa.
Julai 26 akiwa mkoani Singida, Rais Magufuli tena alisema “Haiingii
akilini watu wanakuja wanachukua mali zetu na kuondoka nazo, ifike
mahali tuamke, tumeibiwa vya kutosha, nendeni mkachimbe madini, hizo
fedha tutagawana sisi, hata kama hatufanyi kazi hizo fedha tutagawana.
“Wapo
wachina wanakuja kuchimba barabara hapa nchini, tunashindwaje kuwatumia
hawa wakachimbe madini yetu kisha wakatuachia dhahabu yetu halafu wao
wakaondoka?
“Mimi
ndiye Rais, hakuna anayejua siri za serikali kama mimi na nawaambia
mmepata mtu ambaye anazungumza ukweli, ningeweza kunyamaza kwa vingine
ninavyoviona, lakini nataka kujenga Tanzania mpya.
“Yale
makontena yote ningeweza kuwaambia tugawane mzee, hata kingereza
ninajua, ningeweza kuwaambia give me ten percent (asilimia 10).
“Ningejenga
mahoteli na kuwa na kampuni nyingi kwani wapo Watanzania wamejenga huko
nje lakini nyumba za wazazi wao zimechakaa, mimi nimezaliwa hapa,
ninaishi hapa na nitakufa hapa,” alisema Rais Magufuli.
No comments:
Post a Comment