Monday, July 17, 2017

NABII MKUU MH DK GEODAVIE AWATAKA WATU KUWA NA AKILI ZA ROHONI NA AKILI ZA MWILINI.





Nabii mkuu Mh Dk GeoDavie  amewataka watu kuwa na uwezo mzuri wa akili za rohoni na mwilini ili waweze kufanikiwa katika maeneo mbalimbali maishani.
Nabii mkuu Mh Dk GeoDavie  ameyasema hayo katika ibada ya jiji chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika hema la kukutania kisongo arusha ambapo amesema kila kitu kilichofanyika vizuri huwa kinakuwa na maandalizi mazuri.
Pia amesema kuwa katika maisha watu wanatakiwa waendeshe akili mbili za rohoni na akili za mwilini ili waweze kufanikiwa katika mambo mbalimbali maishani
Katika ibada hiyo Nabii mkuu Mh Dk GeoDavie  ametangaza kuwepo hemani jumapili ijayo ambapo amesema itakuwa ni jumapili ya kusanyiko huku akiwagiza watu kuja na sadaka maalumu  kwa ajili ya kufanyika kichwa kwa akili za rohoni na akili za mwilini.
Nabii mkuu Mh Dk GeoDavie  ametoa wito kwa watu wote kuhudhuria ibada hiyo kwani itakuwa ni siku ya muhimu kwa kila Mtu

Kwa upande wa watu waliohudhuria ibada ya chuo kikuu cha manabii wamesema kuwa wamebarikiwa sana.

No comments:

Post a Comment