Cristiano Ronaldo amemtaka Neymar
kutohamia PSG na kusubiri kwenda Manchester United wakati utakapowadia. (Diario
Gol)
Meneja wa Inter Milan Luciano
Spalletti ameionya Manchester United kwa kusema watoe pauni milioni 48 kama
wanamtaka Ivan Perisic, vinginevyo
wasahau kumsajili winga huyo. (The Sun)
wasahau kumsajili winga huyo. (The Sun)
Arsene Wenger amedai kuwa PSG
wanataka kumsajili Neymar kwa sababu wameshindwa kumsajili Alexis Sanchez.
(Daily Mirror)
Monaco wamesema wanataka pauni
milioni 55 kumuuza winga Thomas Lemar, 21, ambaye anasakwa na Arsenal. (Daily
Star)
Manchester United wapo tayari kuwapa
PSG pauni milioni 70 ili kumsajili kiungo Marco Verratti. (Daily Express)
Marco Verratti amesema chaguo lake
la kwanza ni kwenda Barcelona, ingawa pia yuko tayari kwenda Manchester United.
(Express)
Manchester United wapo tayari
kupanda dau kumtaka kipa chipukizi wa Bolton Wanderers Jake Turner, 18. (The
Sun)
Juventus wameacha kumfuatilia kiungo
wa Chelsea, Nemanja Matic, 28 na hivyo kutoa mwanya kwa Manchester United
kukamilisha uhamisho wake. Chelsea wamesema wanataka pauni milioni 40 ambazo
Juve hawapo tayari kutoa. (Telegraph)
Meneja wa Manchester United Jose
Mourinho ametoa "hakikisho la 100%" kwa mashabiki kuwa kipa David de
Gea atakuwepo Old Trafford msimu huu mpya. (Telegraph)
Manchester United na Arsenal huenda
wakapambana katika kumsajili winga wa Real Madrid Marco Asensio, 21. (Don
Balon)
Deportivo la Coruna wamempa mkataba
wa miaka kumi Lucas Perez katika jitihada za kumshawishi mshambuliaji huyo wa
Arsenal kurejea katika klabu yake hiyo ya zamani. (DXT Campeon)
Mazungumzo ya uhamisho wa
mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28 kwenda PSG yameporomoka kutokana na
bei kubwa ya ada ya uhamisho na mshahara anaodai. (Le Parisien)
Arsenal wanajiandaa kupanda dau la
takriban euro milioni 30 kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho.
(Record)
Chelsea wataongeza bidii katika
kutaka kumsajili kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 23, wiki hii ingawa
huenda wakakabiliwa na ushindani kutoka Manchester City. (Express)
Chelsea wanataka kuwazidi kete
Manchester United na AC Milan katika kumsajili mshambuliaji wa Fluminese
Ricjardlison. (Gianluca Di Marzio)
Jurgen Klopp amesema kiungo wake
Emre Can haendi popote. (Liverpool Echo)
Liverpool wanasubiri kuona kama
Southampton watakuwa tayari kuzungumzia uhamisho wa Virgil van Dujk. (Liverpool
Echo)
West Brom wanajiandaa kutoa pauni
milioni 10 kumsajili beki wa Manchester United Chris Smalling, 27. (Daily Star)
Matumaini ya Liverpool kumsajili
kiungo wa RB Leipzig Naby Keita yamefifia baada ya klabu hiyo kusisitiza kuwa
haumuuzi mchezaji huyo. (Sky Sports)
No comments:
Post a Comment