Korea Kusini
imependekeza kufanyika mazungumzo ya kijeshi na Korea Kaskazini, baada ya
majuma kadhaa ya msukosuko, kufuatia hatua ya Korea Kaskazini ya kufanya
majaribio ya makombora.
Ikiwa mazungumzo hayo
yatafanyika, yatakuwa ndiyo ya kwanza ya juu tangu mwaka 2015.
Maafisa wa vyeo vya
juu walisema kuwa mazungumzo hayo yatalenga kisitisha vitendo vyote vyote
ambavyo huchangia kuwepo misikusuko ya kijeshi katika eneo lenye ulinzi mkali
kati ya Kusini Kaskazini.
Rais wa Korea Kusini
Moon Jae-in tangu mwanzo alikuwa ameashiria kuchukua hatua ya kuleta
ushirikiano wa karibu na Korea Kaskazini.
Haki miliki ya picha Reuters Image
caption Korea Kaskanzini imekuwa ikifanyia makomboa majaribio
Akitoa hotuba hivi
majuzi mjini Berlin, alisema kuwa mazungumzo na Korea Kaskazini yanastahili
kufanyika na kutaka muafaka kuafikiwa.
Lakini hatua za Korea
Kaskazini kuyafanyia majaribio makombora likiwemo la hivi majuzi la masafa
marefu, yanaenda kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa.
Naibu waziri wa
ulinzi nchini Korea Kusini Suh Choo-suk, aliuambia mkutano wa wanahabari kuwa
mazungumzo yatafanyika eneo la Tongilgak, katika jengo la Korea Kaskazini
katika eneo lisilo na ulinzi mkali kati ya nchi hizo mbili.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment