Hatua zote za
kiusalama zilizoweka hivi majuzi mjini Jerusalem, zilizozua maandamano kutoka
kwa wapalestina zimeendolewa kwa mujibu wa polisi nchini Israel.
Viongozi wa dini
katika utawala wa Palestina sasa wataacha kususia eneo hilo takatifu.
Vizuizi hivyo
viliendelelea leo asubuhi, siku mbili baada ya mitambo wa kutambua chuma
kuondolewa.
Mzozo uliibuka baada
ya kuliwa kwa polisi wawili wa Israel karibu wiki mbili
zilizopita.
Israel imesema kuwa
itachukua hatua zisizokuwa na vizuizi miezi sita inayokuja.
Kumekuwa na karibu
makabiliano ya kila siku kati ya vikosi vya usalama vya Israel na waandamanaji
tangu mitambo ya kutambua chuma iwekwe baada ya kuuwawa kwa polisi tare 14 mwezi
huu karibu na eneo linalofahamika kama Haram al-Sharif kwa waislamu na Temple
Mount kwa wayahudi.
Wapalestina wanne
waliuawa na raia watatu wa Israel kuuliwa kwa kuchomwa visu na mpaletina ambaye
alidai alikuwa akilipiza hatua za Israel eneo takatifu.
No comments:
Post a Comment