Ameyasema hayo leo
wakati akiongoza ibada ya jiji katika hema la kukutania chuo kikuu cha manabii
kisongo ambapo maelfu ya watu kutoka sehemu
mbalimbali wamehudhuria ibada hiyo
ya unabii mkuu.
Katika ibada hiyo
Nabii Mkuu amefundisha na kutamka matamko mbalimbali ambayo yalikuwa baraka kwa
wale waliohudhuria ibada hiyo.
Aidha amewataka
watumishi wa Mungu kufanya kazi ya Mungu kwa bidii bila kukubali kuyumbishwa na
kitu chochote katika utendaji kazi wao kwa ajili ya kuijenga serikali ya ufalme
wa Mungu.
Pia Nabii Mkuu Mh
Dk. GeorDavie ametangaza kuwa siku ya tarehe 9/9 mwaka huu anatarajia kufanya
kongamano ambalo litakuwa la Tisa tangu kuanzishwa kwa makongamano katikahuduma
ya Ngurumo Ya Upako.
Pia katika ibada
hiyo Nabii mkuu Mh Dk GeorDavie ametangaza jumapili ya tarehe 13 mwezi wa nane kuwa
siku ya Pipa Day ambapo itafanyika Mjini Mwa Daudi Katika Bonde La Utulivu.
Wakati huo huo Nabii
Mkuu Mh. Dk GeorDavie ametangaza kuwepo radioni siku ya kesho katika kipindi cha kusapoti magurudumu ya Radio
kuanzia majira ya saa mbili na nusu za usiku.
No comments:
Post a Comment