Tuesday, July 25, 2017

WATU WATAKIWA KUWA NA UNYENYEKEVU WA KUTII MAAGIZO.

.Watu wametakiwa kuwa wanyenyekevu kwa kutii maagizo yanayotolewa na  Nabii Mkuu Mheshimiwa  Dk  GeorDavie  ili kufanikiwa katika  changamoto wanazopitia mashani.

Hayo yamesemwa na watumishi wa ngurumo ya upako wakati wakihubiri katika 
chuo cha nabii ibada iliyofanyika siku ya leo kwenye hema la kukutania  kisongo Arusha.
 Mtumishi mwanafunzi Mwajuma Hassani pamoja na Apostel Joyce  wamesema ni vyema watu kushiriki katika  kila jambo ambalo Nabii Mkuu anasema ili waweze kufanikiwa kwa wepesi.
Wamesema maagizo hayo ni kama sadaka maalum,kushiriki katika makongamano mbalimbali pamoja na kushiriki ibada katika chuo cha manabii kisongo Arusha.
Aidha ibada za katikati ya wiki hufanyika kila siku ya jumanne pamoja na alhamsi ambapo watu hukusanyika kwa ajili ya kupokea nguvu ya mungu ambapo watu huudhuria kwa ukaribu zaidi na watumishi wa ngurumo ya upako.
 

No comments:

Post a Comment