Wednesday, July 19, 2017

WAMAMA WATAKIWA KUJIANDAA VYEMA KUPOKEA NGUVU YA MUNGU SIKU JUMAPILI YA TAR.23

Wamama wametakiwa kujiandaa vyema na kuweka maandilizi tayari ili kuweza kupokea nguvu ya mungu na Baraka za mungu zitakazo achiliwa siku ya jumapili katika ibada ya chuo kikuu cha manabii.

Hayo yamesemwa na wamama siku ya jana wakati wakizungumza katika kipindi cha wamama na majukumu kinachorushwa na N.Y.U Radio ambapo wamama hao wamewataka wamama wenzao kuja na waache visingizio vya kukabiliwa na kazi   .
Aidha bi Anna Numi ambaye ni afisa masoko wa N.Y.U Radio amesema
maandalizi ni  jambo la kuzingatia kwa sababu bila maandalizi huwezi kufanya vitu na kufanikiwa.
Kwa upande wake Mchungaji Anna Pita Salanje wa huduma ya ngurumo ya upako amesema kukiwa na kiongozi mzuri lazima kuwe na maandalizi mazuri ya kuyaendea mafanikio  ya kupokea hatua mpya.
Kipindi cha wamama na majukumu ni kipindi ambachio hurushwa na n.y.u redio kila siku ya jumanne kuanzia saa kumi na moja za jioni hadi saa 12 na nusu za jioni ambapo wamama hupata fursa ya kujadili maswala mbalimbali yahusuyo familia.

No comments:

Post a Comment