Pongezi
hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti leo, Julai 17, 2017 jijini Dar es
Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Masjid Ridhwaa, Alhaj Suleiman
Seif Nassor na aliyekuwa mgombea wa CCM wa Ubunge Jimbo la Sengerema
kupitia kura ya maoni, Laurence Mabawa.
Wakati
akizungumza na wanahabari, Alhaj Nassor amesema bodi hiyo imemamua
kumpongea Dkt. Magufuli kutokana na kazi nzuri anayofanya tangu
alipoingia madarakani.
Kwa
upande wake Mabawa, amesema licha ya kumpongeza Rais Magufuli, ameandaa
kampeni kabambe inayojulikana kama ‘Magufuli Baki’ inayotarajiwa
kufanyika hivi karibuni kwenye mikoa yote nchini, ambapo kupitia
mikutano wananchi wenye nia njema watamuomba rais abaki katika msimamo
wake wa kuwatetea wanyonge na masikini.
“Kampeni
ya Magufuli Baki itahusisha mikoa yote ya Tanzania kwa kuwafikia
wananchi wakiwemo wanafunzi wa sekondari kwa kufanya mikutano yenye nia
njema ya kumwomba Rais abaki kwenye msimamo wake, kampeni hii itawapa
fursa wananchi kutoa maoni yao kuhusu utendaji kazi wake iwe kwa
kupongeza au kukosoa,” amesema.
Katika
hatua nyingine, Mabawa amelaani baadhi ya wanasiasa na wananchi
wanaotoa lugha za maudhi na kejeli kwa watu wanaojitokeza hadharani
kumpongeza Rais Magufuli na serikali yake.
“Niombe
TCRA kuwachukulia hatua kali wote wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya
kwa kuwatolea maneno ya kejeli na kuudhi watu wanaojitokeza kumpongeza
Rais,” amesema.
No comments:
Post a Comment