Rais
Magufuli ameitaka kampuni ya Nyanza inayoshughulikia ujenzi wa barabara
ya mkoani Kigoma kuanza kufanya kazi usiku na mchana kwa kuwa wapo
baadhi ya wananchi hawajahi kuona lami maisha yao yote mpaka wanakufa.
Rais
Magufuli ametoa kauli hiyo leo wakati akihutubia wakazi wa Kakonko
mkoani Kigoma katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kibondo mpaka
Nyakanazi yenye urefu wa kilomita 50 kwa kiwango cha lami.
"Wananchi
hawa wanahitaji barabara ya lami wameteseka tangu dunia iumbwe, wako
watu hawajui rangi ya lami, wapo watu hapa wamezaliwa, wamezeeka hawajui
rangi ya lami ikoje. Kwa sababu hawajawahi kuona barabara ya lami
katika maisha yao, kwa hiyo nataka hii lami ianze na mjipange kweli
mfanye kazi usiku na mchana", amesema Rais Magufuli.
Pamoja
na hayo Rais Magufuli amewaagiza makandarasi kufanya kazi ipasavyo na
wasipofanya hivyo watachukuliwa adhabu kali zidi yao.
"Kwa
bahati nzuri mimi kufukuza makandarasi ni kama kunywa chai, sasa asije
akanirudisha kule nilipokuwa kwa sababu sasa ni Baba wa wote lakini
nilipokuwa Waziri nilikuwa nafukuza tu, kwa kupitia bodi ya makandarasi
nilikuwa nafuta wakandarasi na mimi nikuombe Prof. Mbalawa usiwe mpole.
Makandarasi watakao kuwa wanafanya kazi hovyo hovyo, pole pole chukua
'action' ili kusudi kama kashindwa kufanya kazi ya ukandarasi akafanye
nyingine hata ya kuvua samaki", amesisitiza Rais Magufuli.
Kwa
upande mwingine, Rais Magufuli amewataka wananchi kibondo na kasuru wa
mkoa wa Kigoma na watanzania wote kwa ujumla kudumisha ulinzi na usalama
katika maeneo yao wanayoishi ili kupunguza au kumaliza kabisa matatizo
ya kihalifu yanayotokea.
No comments:
Post a Comment