Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli amefunguka na kuahidi kuwa bado ataendelea kuchomoa baadhi ya watu katika vyama vya siasa nchini huku akisema ataacha vilaza tu kwenye vyama hivyo
Ameyasema hayo jana alipokuwa kwenye ziara mkoani Tabora katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi, ambapo alisema kuwa maendeleo ya nchi hayana vyama ndiyo maana ameweza kuchangua baadhi ya viongozi kutokea upinzani na kudai kuwa zoezi hilo litakuwa endelevu.
“Maendeleo
hayana chama ndiyo maana unaona nimeweza kuteuwa baadhi ya viongozi
kutoka tena kwenye chama kidogo, na nitaendelea kuchomoa watu wenye
akili akili kutoka kwenye vyama mbalimbali nitawaacha vilaza huko huko,”alisema Rais Dkt. Magufuli
Hata
hivyo, kwa upande wake, Prof. Kitila Alexander Mkumbo ambaye ni
mwanachama wa ACT- Wazalendo ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maji baada ya kupewa nafasi ya kusalimia wananchi na kutambulishwa
alifunguka na kusema kuwa, Rais Magufuli amevunja mwiko wa Serikali kuwa
ikiongozwa na watu kutoka chama kimoja baada ya kumteua yeye kuwa
Katibu Mkuu wa Maji pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo,
Anna Elisha Mghwira ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment