Thursday, July 20, 2017

WATUMISHI WA MUNGU KUTOKA MAKANISA MBALIMBALI WAENDELEA KUITIKIA WITO WA NABII MKUU TANZANIA MHE. DK. GEORDAVIE.


Watumishi wa Mungu kutoka makanisa mbalimbali wameendelea kuitikia wito uliotolewa na Nabii Mkuu Mh Dk.GeorDavie siku ya Jumapili ya Tarehe 23 mwezi huu kuwa itakuwa Jumapili ya kusanyiko kuu.

Watumishi hao ambao ni Mtume Marco, Nabii Mdogo John pamoja na Mwinjlist Aman Soa, wameyasema hayo katika kipindi cha jukwaa la watumishi kinachorushwa na N.Y.U Radio jioni ya leo.


Pia wamewataka watumishi wengine waliotamkiwa neno na Nabii Mkuu kuhakikisha wanaitikia Wito huo ili kupokea maneno ya kinabii ambayo
yatawawezesha kuendeleza huduma zao.

Watumishi hao wamesema kuwa  ni vyema watu wakatii wito uliotolewa na Nabii Mkuu wahudhurie siku hiyo ambayo itakuwa ni jumapili ya kusanyiko kuu ambapo atawasimika watu katika nafasi mpya na ya Baraka.

Aidha Nabii mkuu Mh Dk. GeorDavie siku ya jumapili ya tarehe 16 mwezi huu alitoa agizo kwa kila mtu anayemwamini, kuja na sadaka maalumu ya Tsh.13,000/= kwa ajili ya kuandama mstari wa 13 unaotoka katika kitabu cha kumbukumbu la Torati 1:13 unaosema:   

'Jitwalieni watu wenye akili na fahamu, watu wanaojulikana, kwa kadiri ya kabila zenu, nami nitawafanya wawe vichwa juu yenu.'

No comments:

Post a Comment