Maseneta wengine
wawili wa chama cha Republican wanasema kuwa wanapinga mpango wa chama
chao, wa kuubadilisha muswada wa afya wa Obamacare hatua iliowawacha
viongozi wa Republican na uchache wa kura kufanya mabadiliko hayo.
Viongozi
wa Republican wanashikilia viti 52 katika bunge hilo lenye wanachama
100, na huku wanachama wawili wa Republican wakiupinga muswada huo
hawangeweza kuruhusu viongozi wengine kuupinga.
Rais Trump aliahidi kuubadilisha muswada wa afya wa rais Obama kama ahadi yake wakati wa kampeni
Maseneta hao wawili walitangaza hatua yao mara moja.
Huku
wakisema kuwa kulikuwa na matatizo mbalimbali kuhusu muswada wa
Obamacare, waliongezea kuwa ''hawawezi kuidhinisha sera mbaya''.
Maseneta wengine wawili, Rand Paul na Susan Collins
Hatua
hiyo inaendeleza kuwatoza kodi muhimu matajiri huku ikiwaondolea mzigo
watoaji huduma za bima ili kuweza kuwapunguzia malipo watu masikini
wanaohitaji huduma ya afya.
Democrats
walikuwa wamesema kuwa hawatakubali kuubadilisha muswada huo wa
Obamacare lakini wanaweza kufanya kazi kwa pamoja ili kuufanya kuwa
imara.
Viongozi wa Republican na ikulu ya Whitehouse sasa
watalazimika kuamua iwapo watauandika upya mpango huo ama kuanzisha
juhudi mpya bila kupendelea chama chochote kuangazia matatizo
yaliopatikana na vyama vyote viwili katika muswada wa Obamacare, ama
kuangazia maswala mengine kama vile mabadiliko ya kodi.
Akiongea kuhusu kile kimetajwa kuwa pigo kubwa ,rais Trump
amewataka Republicans kuubadilisha muswada huo wa Obamacare na kuanza
juhudi za kutengeza muswada mwengine wa afya ambao utaungwa mkono na
Democrats.
Bunge la seneti limekuwa likichelewesha likizo yao kwa
lengo la kubadilisha muswada huo wa aliyekuwa rais wa Marekani Barrack
Obama.
No comments:
Post a Comment