Monday, July 24, 2017

INTERNATIONAL CHAMPIONS CUP: MAN U YAINYUKA REAL MADRID.

Kwenye Mechi ya International Champions Cup iliyochezwa Levi’s Stadium, Santa Clara, California, USA, Manchester United na Real Madrid zilitoka Sare 1-1 katika Dakika 90 za Mchezo na Mshindi kupatikana kwa Mikwaju ya Penati ambapo Man United walishinda kwa Penati 2-1.
Man United walifunga Bao Dakika ya 46 ya Kipindi cha Kwanza baada Anthony Martial kuwapita Mabeki Watatu na kumpa Mpira Jesse Lingard alieukwamisha Mpira wavuni.
Manchester United yaizamisha Real Madrid kwa mikwaju ya penalti
Hadi Haftaimu, Man United 1 Real Madrid 0.
Kipindi cha Pili kilianza kwa Timu zote kubadili Vikosi vyao.
Katika Dakika ya 52, Man United walilazimika kumtoa Ander Herrera
alieumizwa Goti na kumuingiza Chipukizi Scott McTominay.
Real walisawazisha Dakika ya 69 kwa Penati ya Casemiro, Penati iliyotolewa kufuatia Rafu ya Victor Lindelof kwa Theo Hernandez.
Bao hizo 1-1 zilidumu hadi Mpira kumalizika na Mshindi kuamuliwa kwa Tombola ya Penati Tano Tano.
Kwenye Mikwaju hiyo, Man United walifunga Penati zao 2 kupitia Daley Blind na Henrikh Mkhitaryan wakati Martial, McTominay na Lindelof wakikosa.
Real walifunga Penati yao kupitia Luis Sanchez na waliokosa ni Kovacic, Amaiz, Hernandez na Casemiro.
================
Kifuta Jasho.
-Hii ni Mechi ya 12 kati ya Man United na Real Madrid.
-Ushindi Real 4 Man United 4, Sare 4
===============
Mbali ya Mechi hii ya Kirafiki, Timu hizi zitapambana tena Agosti 8 huko nchini Macedonia kugombea UEFA SUPER CUP Kombe ambalo hushindaniwa na Bingwa wa UEFA CHAMPIONZ LIGI na yule alietwaa UEFA EUROPA LIGI.
Real walitwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa kuitwanga Juventus 4-1 na Man United kubeba UEFA EUROPA LIGI kwa kuifunga Ajax Amsterdam 2-0.
VIKOSI VILIVYOANZA:
Real Madrid: Keylor Navas; Daniel Carvajal, Marcelo, Raphael Varane, Nacho; Toni Kroos, Luka Modric, Isco; Karim Benzema, Lucas Vázquez, Gareth Bale
Manchester United: Sergio Romero; Timothy Fosu-Mensah, Matteo Darmian, Eric Bailly, Phil Jones; Michael Carrick, Jesse Lingard, Marouane Fellaini, Andreas Pereira; Anthony Martial, Marcus Rashford

 


No comments:

Post a Comment