Tuesday, July 18, 2017

WATU WALIOTOWEKA MWAKA 1942 WAPATIKANA KWENYE BARAFU USWISI

The spot where the two bodies were found in glacier

Barafu inayoyeyuka nchini Uswisi imefichua miili miwili inayoaminiwa kuwa ya mtu na mkewe waliotoweka miaka 75 iliyopita.
Marcelin na Francine Dumoulin walitoweka wakati walienda kuchunga ng'ombe
wao katika milima ya Alps mwaka 1942.

Watu hao walikuwa na watoto saba.

Mtoto wao wa mwisho wa kike ambaye sasa ana umri wa 79, anasema habari hizo zimemletea utulivu na anataka kuwafanyia maziko mema.
"Tulitumia maisha yetu yote kuwatafuta," alisema Marceline Udry-Dumoulin.
Uchunguzi wa DNA unatarajiwa kufanywa.
Polisi wanasema kuwa miili hiyo iligunduliwa wiki iliyopita katika eneo la Tsanfleuron na mfanyakazi kutoka kampuni ya kuteleza kwa barafu ya Glacier 3000.

No comments:

Post a Comment