Akielezea tukio hilo, Mkuu wa
Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi
Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 19, julai, 2017
saa mbili usiku katika eneo la Utende kata ya Ikwiriri,
wilaya
Rufiji kanda maalum ya Polisi Rufiji.
“Askari Polisi wa
doria waliwatilia mashaka watu wanaokadiliwa kuwa watano ambapo
walipoanza kuwafutilia ndipo walianza kukimbia huku wakiwashambulia
askari kwa risasi.
"Askari nao kwa ujasiri
walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi wahalifu
wawili miongonio mwao ambao baadaye walifariki wakipelekwa
Hospitali ya Taifa ya muhimbili kutokana na kuvuja damu iliyosababisishwa
na majeraha ya risasi waliyoyapata”
alisema Sabas.
Aliongeza kuwa katika eneo hilo la tukio ilipatikana silaha moja aina ya rifle 375 ambayo ilikutwa imekatwa kitako na mtutu ikiwa na risasi mbili (2). Aidha, Miili ya marehemu wote wamehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Taifa ya muhimbili.
Kamanda sabas ameendelea kutoa
wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa
taarifa zitakazosaidia kukamatwa wahalifu wengine waliosalia na kwamba
opereheni hiyo ya kuwasaka wahalifu katika Kanda hiyo ya kipolisi Rufiji
ni endelevu na hakuna atakayebaki.
No comments:
Post a Comment