Amesema
kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Meli hizo zilizogharimu sh. bilioni
11.253 ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. John Magufuli alizozitoa
ikiwa na lengo la kutatua changamoto ya usafiri wa abiria na mizigo
katika Ziwa Nyasa.
Amesema
kuwa ni jambo la faraja na la kujivunia kwa Serikali na wananchi kwa
pamoja kushuhudia meli zilizotengenezwa na Mtanzania, zikiwa
zimekamilika tayari kwa kuanza kazi ya kuwahudumia wananchi, ambapo
awali suala hilo
lilikuwa likifanywa na raia wa kigeni.
lilikuwa likifanywa na raia wa kigeni.
Waziri
Mkuu amezindua meli hizo zilizojengwa na kampuni ya Kitanzania ya M/S
Songoro Marine Transport jana katika bandari ya Kiwira wilayani Kyela
akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya.
Aidha,
alisema kuwa Meli hizo zitumike katika kukuza uchumi wa wananchi kwa
kusafirisha mizigo na biashara halali kati ya nchi za Tanzania na Malawi
na zisitumike kama eneo la kuingiza wahamiaji haramu pamoja na dawa za
kulevya nchini.
“Changamoto
ya usafiri wa mizigo katika ziwa Nyasa itakuwa historia kwani meli hizi
zitarahisisha usafiri na kupanua wigo wa biashara kati ya Tanzania nan
chi za Malawi na Msumbiji, hivyo tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt.
Magufuli kwa kutoa ahadi hii ambayo leo utekelezaji wake umekamilika.”
Kwa
upande wake, Naibu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)
anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Karim Mataka alisema kuwa ujenzi
wa meli hizo ulianza Juni 2015 na zina uwezo wa kubeba tani 1,000 za
mizigo kwa kila moja.
No comments:
Post a Comment