Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 25 Julai, 2017 amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku 7 katika
Mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora na Singida kwa kufungua barabara ya
Itigi – Manyoni Mkoani Singida.
Barabara
hiyo inayounganisha Mikoa ya Singida, Tabora na Kigoma ina urefu wa
kilometa 89.3 na imejengwa gharama ya Shilingi Bilioni 114.692, fedha
ambazo zimetolewa na Serikali ya Tanzania.
Akizungumza
na wananchi wa Itigi katika sherehe za ufunguzi wa barabara hiyo Mhe.
Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli, amesema
Watanzania wana kila sababu ya kutembea kifua mbele kwa kuwa barabara
hiyo pamoja na nyingine saba alizozifungua katika ziara hii zenye urefu
wa jumla ya kilometa 707 zimejengwa kwa gharama ya Shilingi
Bilioni 806, fedha zote zikiwa zimetolewa na Serikali ya Tanzania.
Bilioni 806, fedha zote zikiwa zimetolewa na Serikali ya Tanzania.
Mhe.
Rais Magufuli amebainisha kuwa miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara
imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini
na kwamba Serikali imeamua kuanzisha Wakala wa Barabara Vijijini kwa
lengo la kuhakikisha barabara za vijijini zinajengwa kwa kiwango cha
lami.
Kwa
barabara ya Mkiwa – Itigi yenye urefu wa kilometa 57 na ambayo tayari
zabuni ya ujenzi ilishatolewa kwa mkandarasi ili aijenge kwa kiwango cha
lami kwa gharama ya Shilingi Bilioni 104, Mhe. Rais Magufuli ameiagiza
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuupitia upya mkataba wa
ujenzi wa barabara hiyo kwa kuwa kiwango cha fedha kilichopangwa ni
kikubwa ikilinganishwa na gharama halisi.
Pia
amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa Mnyaa kujadiliana na Mkandarasi anayejenga barabara hiyo ili
aweze kuendelea kujenga barabara kutoka Itigi kuelekea Chunya hadi
Makongorosi Mkoani Mbeya.
Pamoja
na wananchi wa Itigi Mkoani Singida, Mhe. Dkt. Magufuli aliyetokea
Tabora amezungumza na wananchi waliosimamisha msafara wake katika vijiji
vya Kigwa, Kizengi na Tura Wilayani Uyui na amewataka kuendelea kuchapa
kazi kwa juhudi na maarifa pamoja na kuzingatia uzalishaji mazao
yanayostahimili ukame kama vile uwele, mtama, viazi na muhogo ili
kuepuka tatizo la upungufu wa chakula.
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli amewataka viongozi wote nchini kuhamasisha wananchi
kufanya kazi hususani shughuli za kilimo ambacho ni uti wa mgongo wa
Taifa, na ameonya kuwa kiongozi ambaye hatatekelezi agizo hilo atakuwa
hafai na ataondolewa.
“Nawaagiza
Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya hamasisheni watu kufanya kazi na kama
kuna viongozi na watendaji wasiotekeleza wajibu huo katika maeneo yenu
waondoeni mara moja” ameagiza Mhe. Rais Magufuli.
Viongozi
wengine waliongozana na Mhe. Rais Magufuli katika ziara ya leo ni Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis
Kigwangalla, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu
Prof. Norman Sigalla King na Wabunge wa Mkoa wa Singida.
Mhe. Rais Magufuli amewasili katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment