Sunday, July 30, 2017

MAREKANI NA KOREA KUSINI WAJIPANGA KWAAJILI YA KOREA KASKAZINI.

Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema kuwa Marekani itaweka zana maalumu za ulinzi Korea Kusini kama hatua ya ilani muhimu kwa Korea Kaskazini ambayo imefanya zoezi la kombora la masafa marefu la kutoka bara moja hadi jingine katika jaribio la pili sawa na hilo chini ya muda wa mwezi mmoja.

Korea Kaskazini imethibitisha kuwa ilifaulu kufyatua kombora la pili aina hiyo chini ya usimamizi wa kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un.
Kombora hilo lilionekana kuwa na nguvu zaidi kuliko lile la kwanza.
Kombora hilo lililoanguka karibu na ufuo wa Japan limeshutumiwa kimataifa huku Rais Donald Trump akisema jaribio hilo lilifanywa kiholela na ni hatari.
Kombora hilo lilionekana kuwa na nguvu zaidi kuliko lile lililojaribiwa mapema mwezi huu kwa kuwa lilikuwa angani kwa zaidi ya dakika 47, kulingana na taarifa zilizotolewa na Pyongyang na ambapo lilienda kwa mwendo wa kilomita 1,000. Lilidondoka karibu na Ufuo wa Japan.
Vikosi vya kijeshi vya Marekani na Korea Kusini vilivanya zoezi la kijeshi kwa pamoja ambapo makombora kadhaa yalilipuliwa na wizara ya ulinzi kutangaza kuwa silaha maalumu zitawekwa nchini humo.
Vifaa vingine vilivyoonyeshwa katika zoezi hilo na meli maalumu za kubeba ndege za kivita viliichukuliwa kama hatua ya kuonya Pyongyang.

No comments:

Post a Comment