Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu, (LHRC) kimetoa taarifa yake kwa vyombo
vya habari kikisikitishwa na jinsi Bunge, lilivyotengua uteuzi wa
wabunge wa viti Maalum juzi.
“LHRC inafuatilia mwenendo wa demokrasia nchini na kinatambua uwepo wa mzozo wa kiutawala ndani ya CUF, mzozo ambao umepelekea mgawanyiko ndani ya chama hicho na kufikia hatua ya wanachama kufikishana mahakamani kwa ajili ya usuluhishi,” imesema.
Taarifa
hiyo iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Anna Henga imesema LHRC
ilitaraji kuona Bunge likiheshimu mhimili wa mahakama ambao bado
haujatolea uamuzi shauri la Bodi ya Wadhamini ya CUF dhidi ya maamuzi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa ya kumtambua Profesa Lipumba kama
mwenyekiti.
“Kwa
maamuzi haya bunge limedharau mhimili wa mahakama ambacho ni chombo
huru kwa mujibu wa Katiba. LHRC kinalitaka Bunge kurejea maamuzi yake na
kusitisha maamuzi hayo mpaka mahakama itakapochukua hatua.” Imesema taarifa hiyo.
No comments:
Post a Comment