Rais
John Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vyote vya mafuta
nchini, kuhakikisha wanaweka na kutumia mashine za kielektroniki za
kutolea risiti (EFD) na atakayekiuka agizo hilo atafutiwa leseni ya
biashara yake.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Kigoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa KM 154 huku akiwataka mawaziri wenye dhamana kuhakikisha wanafuatilia maagizo hayo kuanzia sasa.

"Wanaolalamika kukosa mafuta waendelee kufanya hivyo, ni mara mia tukose mafuta kuliko kuwa na wafanyabiashara wanaokwepa kodi", amesema Rais Magufuli.
Kwa
upande mwingine, Rais Magufuli amepiga marufuku wananchi kutozwa kodi
kwa mzigo wenye uzito wa tani moja anapousafirisha kutoka wilaya moja
kwenda nyingine.
No comments:
Post a Comment