Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa
Tanzania siyo lango la kupitishia dawa za kulevya kwenda nchi za nje
hivyo ameagiza ulinzi uimarishwe katika mipaka yote ya nchi na kuwa wale
watakaobainika watachukuliwa hatua kali.
Majaliwa
amesema hayo wakati akizungumza na watumishi wa kituo cha forodha cha
Kasumulu kilichopo mpakani mwa Tanzania na Malawi wilayani Kyela,.
Amesema
kuwa kunatabia ya baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu kuitumia Tanzania
kama njia ya kupitisha dawa za kulevya kwa ajili ya kupeleka nchi
za Afrika ya Kusini, Malawi na Zambia.
za Afrika ya Kusini, Malawi na Zambia.
“Endeleeni
kufanya upekuzi wa kina wa magari, watu na mizigo yote yote katika
mipaka yetu. Tanzania siyo lango la kupitishia dawa za kulevya na
Serikali haitakubaliana na jambo hilo.”
Aidha,
Majaliwa amewataka viongozi hao kuhakikisha biashara zote za magendo
zinazofanyika mipakani, zikiwemo za kubadilisha fedha zinadhibitiwa kwa
kuwa zinaikosesha Serikali mapato.
Hata
hivyo, ameongeza kuwa ni vema yakawepo maduka ya kubadilishia fedha
katika maeneo hayo ili kudhibiti biashara hiyo ambayo kwa sasa inafanywa
kimagendo huku Serikali ikikosa kodi.
No comments:
Post a Comment